89 – Abu Sa´iyd al-Ashajj ametukhabarisha: ´Amr bin Qays bin Yasiyr bin ´Amr ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Katisha na mpumbavu.” [1]

90 – Abu Hishaam ar-Rifaa´iy ametukhabarisha: Ibn Yamaan ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha: Habiyb bin Abiy Thaabit ametukhabarisha: Maymuun bin Abiy Shabiyb amenihadithia, kutoka kwa ´Aaishah, ambaye amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alituamrisha kuamialiana na watu kulingana na nafasi zao.”[2]

91 – Ibn Abiy Shaybah ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Idriys ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn ´Ajlaan, kutoka kwa Ibraahiym bin Murrah, kutoka kwa Ibn Shihaab, ambaye amesimulia kuwa ´Umar amesema:

“Usisuhubiane  na muovu akaja kukufundisha maovu yake. Usimweleze siri zako pia.”

92 – Ibraahiym bin al-Hajjaaj ametukhabarisha: Salaam ametukhabarisha, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa ´Umar, ambaye amesema:

“Yeyote anayeingia kwa lango la uovu atatuhumiwa.”

93 – ´Abdul-Wahhaab bin Najdah ametukhabarisha: Abu ´Amr bin Bukayr bin Diynaar ametukhabarisha, kutoka kwa Abudh-Dhwayyaal, ambaye amesema:

“Jifunze ukimya kama unavyojifunza maneno. Ikiwa maneno yanakuongoza, basi ukimya unakulinda. Ukimya una sifa mbili: Unakusaidia kuepuka ujinga kwa yule ambaye ni mjinga zaidi yako na unakusaidia kujifunza elimu kutoka kwa mwenye elimu zaidi yako.”

Ameelezea pia kwamba Abudh-Dhayyaal amesema:

“Jifunze kusema kuwa hujui na wala usijifunze kusema kuwa unajua. Ukisema kuwa unajua basi watakuuliza mpaka hutojua tena, ukisema kuwa hujui watakufundisha mpaka ujue.”

[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (889).

[2] Abu Daawuud (4842). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (4842).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 29/06/2025