11. Je, unatukuza maharamisho ya Allaah?

Miongoni mwa alama za kumtukuza Allaah katika mambo yaliyokatazwa, ni bidii ya kujiepusha na mahali au sababu zinazoweza kumpelekea mtu kutenda maasi, pamoja na kila njia inayomkaribisha huko. Ni kama mfano wa mtu anayekimbia maeneo yenye picha au sura zinazoweza kumfitini kwa kuogopa kutumbukia katika fitina hiyo. Mfano mwingine ni mtu kujiepusha na vitu vyenye madhara ili asitumbukie katika jambo lisilo na madhara, kujiepusha na mambo yaliyoruhusiwa kupita kiasi kwa kuchelea asije kutumbukia katika yaliyochukizwa na kujiepusha na watu wanaofanya maasi hadharani, wakayapamba, wakayalingania, wakayaviondolea uzito na wasijali madhara yake, kwani kuandamana na watu wa namna hii kunaongoza katika ghadhabu na hasira ya Allaah (Ta´ala). Hawezi kushirikiana nao isipokuwa mtu ambaye ndani ya moyo wake kumeondoka kuheshimu na kutukuza mipaka ya Allaah.

Katika alama za kumtukuza Allaah kwa yale aliyoyakataza ni kwamba mtu anapoona mipaka ya Allaah (Ta´ala) imekiukwa basi huona ghadhabu kwa ajili ya Allaah na moyoni mwake hujawa na huzuni na udhalilifu pindi Allaah (Ta´ala) anapoasiwa katika ardhi Yake na hukosa nguvu ya kusimamisha mipaka na amri Zake wala hawezi yeye mwenyewe kubadilisha hali hiyo.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 26
  • Imechapishwa: 30/07/2025