Kila mmoja anataka Pepo ambazo chini yake kunapita mito. Hakuna yeyote anayetaka Moto na adhabu. Lakini kinachozungumziwa ni kufanya zile sababu zinazomfikisha mtu Pepo na kumuokoa na Moto. Hakuna sababu nyingine isipokuwa kulazimiana na Salaf. Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

”Mwisho wa ummah huu hautotengemaa isipokuwa kwa yale yaliyowatengeneza wa mwanzo wao.”[1]

Kipi kilichowatengeneza wa mwanzo wao? Ni Qur-aan na Sunnah. Mwisho wa ummah huu hautotengemaa isipokuwa kwa Qur-aan na Sunnah. Qur-aan na Sunnah vipo na himdi zote njema anastahiki Allaah. Vimehifadhiwa kwa hifdhi ya Allaah:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi Tumeteremsha Ukumbusho na hakika Sisi bila shaka ndio Tutakaoihifadhi.”[2]

Vimehifadhiwa kwa idhini ya Allaah. Yeyote mwenye kuvitaka kwa ukweli na akajifunza navyo mafunzo sahihi basi atafikia malengo. Kuhusu anayedai bila ya uhakika au akamfata kichwa mchunga anayedai Salafiyyah ilihali hafuati mfumo wa Salaf, hakumsaidii kitu. Kinyume chake kutamdhuru. Tatizo tu ni kwamba mtu huyu anajinasibisha na Salaf na Slafiyyuun, jambo ambalo ni uwongo na kuwazulia Salaf na Salafiyyah. Huku ni kuwatia watu mchanga wa machoni. Ni mamoja amekusudia kufanya hivo au hakukusudia. Ima ni mzushi au mjinga:

Madai yasiyosimamishiwa hoja

yanabaki kuwa ni madai

[1] Ameyanukuu Qaadhwiy ´Iyaadhw katika ”as-Shafaa” (02/88) na Ibn Taymiyyah katika ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (27/118) na ash-Shaatwibiy katika ”al-I´tiswaam” (01/274).

[2] 15:09

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Salafiyyah haqiyqatuhaa wa simaatuhaa, uk. 36-38
  • Imechapishwa: 06/05/2024