49 – Imaam Ahmad aliulizwa juu ya mtu anayesema kuwa Allaah yuko pamoja nasi na anasoma:

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ

“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao.”

Akajibu: ”Huyo ni Jahmiy. Wanachukua sehemu ya mwisho ya Aayah na wanaacha sehemu yake ya mwanzo. Msomeeni:

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا

“Je, huoni kwamba Allaah Anajua yale yote yaliyomo mbinguni na yale yote yaliyomo ardhini? Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala [hauwi mnong’ono wa] chini kuliko ya hivyo, na wala wa wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao popote watakapokuwa?”[1]

Ujuzi uko pamoja nao. Vilevile amesema (Tabaarak wa Ta´ala):

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ ۖ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ

“Hakika Tumemuumba mwanaadamu na tunajua yale  yanayomshawishi nafsi yake na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingo.”[2]

Ujuzi Wake uko pamoja nao.

50 – Hanbal amesimulia kuwa Imaam Ahmad aliulizwa kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا

“… Yeye Yu pamoja nao popote watakapokuwa.”

ambapo akajibu:

”Ujuzi Wake umekizunguka kila kitu na wakati huohuo Yuko juu ya ´Arshi, pasi na maelezo wala mpaka.”[3]

51 – al-Muzaniy amesema:

”Yuko juu ya ´Arshi kwa utukufu Wake na dhati Yake. Yuko karibu na viumbe Wake kwa ujuzi Wake.”[4]

52 – Imaam Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr amesema:

”Wanazuoni wa Maswahabah na wanafunzi wao wameafikiana kufasiri maneno Yake (´Azza wa Jall):

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا

“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala [hauwi mnong’ono wa] chini kuliko ya hivyo, na wala wa wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao popote watakapokuwa.”[5]

kisha akasema: ”Yuko juu ya ´Arshi Yake na ujuzi Wake uko kila mahali. Hakuna mtu anayetambulika anayeona kinyume.”[6]

53 – Muhammad bin Jariyr at-Twabariy, al-Baghawiy, ath-Tha´labiy na Abu Bakr an-Naqqaash katika tafsiri zao za Qur-aan wamesema mfano wa hayo.

[1] 58:7

[2] 50:16

[3] Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah (3/387-402).

[4] as-Sunnah, uk. 11-13.

[5] 58:7

[6] at-Tamhiyd (7/138-139).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 64-67
  • Imechapishwa: 03/06/2024