Lau mtu atasema kuwa Allaah ndiye muabudiwa na kwamba yeye anampwekesha na kumuabudu Allaah haina maana ya kwamba anakuwa muumini papohapo. Hii sio Tawhiyd. Haitoshelezi kumuabudu Allaah peke yake. Bali ni lazima ukanushe ´ibaadah anayofanyiwa kila asiyekuwa Allaah. Kwa msemo mwingine ni kwamba ni lazima ulete ukanushaji na uthibitishaji.
Neno “Hakuna mungu isipokuwa Allaah” maana yake ni kwamba hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Ikiwa mtu atasema kuwa yeye anamuabudu Allaah peke yake ina maana ya kwamba anakuwa mpwekeshaji? Hapana. Haitoshelezi kule kumuabudu Allaah peke yake. Ni lazima kumuabudu Allaah sambamba na hilo ukanushe ´ibaadah anazofanyiwa asiyekuwa Allaah. Huku ndio kukufuru Twaaghuut. Hili halipatikani isipokuwa kwa ukanushaji na uthibitishaji; “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Kwa hivyo dalili ya kichenguzi hichi cha tatu ni Kauli ya Allaah (Ta´ala):
فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا
“Basi atakayemkanusha twaaghuwt [miungu ya uongo] na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika.”
Kalima ya Tawhiyd “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” ndani yake mna Takhliyah na Tahliyah. Nini maana yake? Takhliyah maana yake ni wewe ukanushe ´ibaadah anazofanyiwa asiyekuwa Allaah. Baada ya kukanusha na kukaripia ´ibaadah za kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah ndipo kunakuja sasa Tahliyah na kumthibitishia ´ibaadah Allaah (´Azza wa Jall).
Neno “Hakuna mungu wa haki… ” hii ndio Takhliyah ikiwa na maana ya kwamba umekanusha ´ibaadah zote anazofanyiwa asiyekuwa Allaah. Nenoo “… isipokuwa Allaah” hii ndio Tahliyah ikiwa na maana ya kwamba umemthibitishia ´ibaadah Allaah pekee. Neno “Hakuna mungu wa haki… ” ndio kukufuru Twaaghuut. Neno “… isipokuwa Allaah” ndio kumuamuni Allaah.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 27
- Imechapishwa: 15/04/2023

Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 27
Imechapishwa: 15/04/2023
https://firqatunnajia.com/11-haitoshelezi-kwa-mtu-kumuabudu-allaah-peke-yake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)