11. Hadiyth “´Umrah moja hadi ´Umrah nyingine ni kafara kwa madhambi yaliyoko baina yake… ”

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“´Umrah moja hadi ´Umrah nyingine ni kafara kwa madhambi yaliyoko baina yake na Hajj yenye kukubaliwa haina malipo mengine isipokuwa Pepo.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Hii Hadiyth ni dalili ya fadhilah ya Hajj yenye kukubaliwa na ujira wake mkubwa mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kwani mwenye kuitekeleza kwa hali hiyo atakuwa miongoni mwa waliopata radhi za Allaah na Pepo Yake.

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) pia amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa:

“Ni kitendo gani kilicho bora zaidi?” Akasema: “Kumwamini Allaah na Mtume Wake.” Akaulizwa: “Kisha kipi?” Akasema: “Kupambana Jihaad katika njia ya Allaah.” Akaulizwa: “Kisha kipi?” Akasema: “Hajj yenye kukubaliwa.”[2]

Kuna maafikiano juu yake.

[1] al-Bukhaariy (1683) na Muslim (1349).

[2] al-Bukhaariy (16, 1447) na Muslim (83).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 18
  • Imechapishwa: 10/05/2025