11. Hadiyth ”Nilimuona Mtume wa Allaah akiswali akiwa peku… ”

al-Bayhaqiy (2/431) amesema: Abul-Husayn bin Bishraan al-´Adl ametufahamisha Baghdaad: Ismaa´iyl bin Muhammad as-Swaffaar ametuhadithia: Sa´daan bin Naswr ametuhadithia: Abu Badr ametuhadithia, kutoka kwa Ziyaad bin Khaythamah, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Iysaa, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Atwaa’, kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa), ambaye amesema:

”Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali akiwa peku na amevaa viatu, akinywa akiwa amekaa na amesimama, akimaliza kuswali anageuka kulia au kushoto, pasi na kujali anafanya hivo upande gani.”

al-Haythamiy amesema kuhusu Hadiyth:

”Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw”. Wanaume wake ni wenye kuaminika.”[1]

Tofauti pekee iliopo ni kwamba imekuja katika kitabu chake ”na anaondoka zake” badala ya ”akimaliza kuswali anageuka kulia… ”

[1] Majma´-uz-Zawaa’id (2/55).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 13
  • Imechapishwa: 02/06/2025