Download

224-

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hamtoingia Peponi mpaka muamini na wala hamtoamini mpkaa mpendane. Je, nisikujulisheni jambo ambalo mtakapolifanya mtapendana? Enezeni salamu kati yenu.”[1]

225-

“Mambo matatu atayeyakusanya basi atakuwa amekusanya imani; inswafu ya nafsi yako, kutoa salamu kwa watu wote na mtu kujitolea ingawa riziki imebana kidogo.”[2]

226-

´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamba kuna bwana mmoja alimuuliza Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Uislamu upi bora ambapo akajibu:

“Kulisha chakula na kumsalimia unayemjua na usiyemjua.”[3]

[1] Muslim (01/74) na wengineo.

[2] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (01/82) kutoka kwa ´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh) hali ya kuishilia kwa Swahabah na kukatika cheni ya wapokezi wake.

[3] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (01/55) na Muslim (01/65).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 06/05/2020