219-
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi.”[1]
220-
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Msilifanye kaburi langu kuwa ni mahali pa kutembelea mara kwa mara na niswalieni. Kwani hakika swalah zenu zinanifikia popote mlipo.”[2]
221-
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Bakhili ni yule nitakayetajwa mbele yake na asiniswalie.”[3]
222-
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Allaah anao Malaika wanaozunguka ardhini wanaonifikishia salamu kutoka kwa Ummah wangu.”[4]
223-
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakuna yeyote anayeniswalia isipokuwa Allaah hunirudishia roho yangu ili niweze kumwitikia salamu.”[5]
[1] Muslim (01/288).
[2] Abu Daawuud (02/218) na Ahmad (02/367). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Abiy Daawuud” (02/383).
[3] at-Tirmidhiy (05/551) na wengineo. Tazama “Swahiyh al-Jaamiy’” (03/25). Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/177).
[4] an-Nasaa´iy (03/43) na al-Haakim (02/421). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-un-Nasaa´iy”.
[5] abu Daawuud (2041). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Abiy Daawuud” (01/383).
- Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huswn-ul-Muslim
- Imechapishwa: 06/05/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)