Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Kwa sababu kila kundi lina sanamu ambalo wanataka wahukimiwe nalo, ingawa wameamrishwa walikufuru. Wanafalsafa hawa wamefanana na wale ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema juu yao:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْاْ إِلَى مَا أَنزَلَ اللّهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَآؤُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللّهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلاَّ إِحْسَانًا وَتَوْفِيقًا

“Je, huwaoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, namna ambavyo wanataka wahukumiane kwa hukumu za kishaytwaan na hali wameamrishwa wakanushe hiyo? Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali. Na wanapoambiwa: “Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume”, utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko. Basi itakuwaje utakapowafika msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao, kisha wakakujia wakiapa: “Hatukutaka isipokuwa mazuri na mapatano”.”[1]

MAELEZO

Kila mpotofu katika watu hawa anaye anayechupa mipaka juu yake, naye ni yule anayehukumu kwa yale ambayo hakuteremsha Allaah. Kila kundi wana kiongozi ambaye wanayachukua maneno yake na wanahukumiwa naye pasi po yale aliyoteremsha Allaah. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَتَوْفِيقًا

“Je, huwaoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, namna ambavyo wanataka wahukumiane kwa hukumu za kishaytwaan na hali wameamrishwa wakanushe hiyo?”

Viongozi wao ndio wanaochupa mipaka kwao. Kwa sababu wanahukumu kwa usiyokuwa Wahy; wanahukumu kwa akili zao, falsafa na fikira zao.

[1] 4:60-62

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 151
  • Imechapishwa: 04/09/2024