105. Hakubadilishwi kitu kilichoandikwa katika Ubao uliohifadhiwa

Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

86 – Endapo viumbe wote watakusanyika kuzuia kitu ambacho Allaah (Ta´ala) amekwishahukumu kutokea kwake, basi hawatoweza. Na endapo wote watakusanyika kukileta kitu ambacho Allaah (Ta´ala) hajahukumu kutokea kwake, basi hawatoweza.

MAELEZO

Hakuna yeyote anayeweza kubadilisha yale aliyoyaandika Allaah katika Ubao uliohifadhiwa. Lau viumbe wote watakusanyika kubadilisha kitu ambacho Allaah amekwishakiandika, basi hawatofanikia, na lau wote watakusanyika kukileta kitu ambacho Allaah hakukiandikia kwenye Ubao uliohifadhiwa, basi hawatoweza. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jua ya kwamba ikiwa taifa zima litaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika isipokuwa kwa kitu alichokwishakuandikia Allaah. Kadhalika wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, basi howatokudhu isipokuwa tu kwa kitu alichokwishakuandikia. Kwani kalamu zimeshanyanyuliwa na sahifa zimeshakauka.”[1]

Hakuna mabadiliko wala mageuzi wa yale aliyoyaandika Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika Ubao uliohifadhiwa.

[1] Ahmad (1/307) na at-Tirmidhiy (2516) ambaye amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 117
  • Imechapishwa: 05/11/2024