al-Qummiy amesema wakati alipokuwa akiifasiri Aayah:
وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا
“Hakika mmeshateremshiwa katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa mzaha, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao. Hakika Allaah atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Moto.”[1]
Aayah za Allaah ni Qur-aan ambayo Allaah ameiteremsha kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kuwaongoza watu. Ambazo ziko na Tawhiyd na kuipiga vita shirki, upotevu, ujinga, kubainisha yaliyo ya halali na yaliyo ya haramu na tabia njema na kutahadharisha uongo na kumzulia Allaah uongo na kukipotosha Kitabu Chake, kama wafanyavyo mayahudi. Kadhalika Raafidhwah wanafuata nyayo za mayahudi.
Wale wanaozifanyia mzaha Aayah za Allaah walikuwa ni makafiri wa Makkah na al-Madiynah kabla hata maimamu hawajazaliwa. Wale wanaozichezea shere Aayah za Allaah baada ya kufa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Raafidhwah Baatwiniyyah. Ni mara ngapi wanazichezea shere Aayah za Allaah kukiwemo mzaha huu ambao tumeufichua hapa! Si washirikina, mayahudi wala maadui wengine wa Allaah hakuna ambao wamezifanyia mzaha Aayah za Allaah sana kama walivofanya hawa Raafidhwah Baatwiniyyah!
[1] 04:140
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 151-152
- Imechapishwa: 12/01/2018
al-Qummiy amesema wakati alipokuwa akiifasiri Aayah:
وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا
“Hakika mmeshateremshiwa katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa mzaha, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao. Hakika Allaah atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Moto.”[1]
Aayah za Allaah ni Qur-aan ambayo Allaah ameiteremsha kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kuwaongoza watu. Ambazo ziko na Tawhiyd na kuipiga vita shirki, upotevu, ujinga, kubainisha yaliyo ya halali na yaliyo ya haramu na tabia njema na kutahadharisha uongo na kumzulia Allaah uongo na kukipotosha Kitabu Chake, kama wafanyavyo mayahudi. Kadhalika Raafidhwah wanafuata nyayo za mayahudi.
Wale wanaozifanyia mzaha Aayah za Allaah walikuwa ni makafiri wa Makkah na al-Madiynah kabla hata maimamu hawajazaliwa. Wale wanaozichezea shere Aayah za Allaah baada ya kufa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Raafidhwah Baatwiniyyah. Ni mara ngapi wanazichezea shere Aayah za Allaah kukiwemo mzaha huu ambao tumeufichua hapa! Si washirikina, mayahudi wala maadui wengine wa Allaah hakuna ambao wamezifanyia mzaha Aayah za Allaah sana kama walivofanya hawa Raafidhwah Baatwiniyyah!
[1] 04:140
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 151-152
Imechapishwa: 12/01/2018
https://firqatunnajia.com/104-al-qummiy-upotoshaji-wake-wa-kumi-na-tatu-wa-an-nisaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)