Adhabu ya kaburi inakuwa kwenye kiwiliwili na roho vyote viwili, roho peke yake au kiwiliwili tu? Je, kiwiliwili kinashirikiana na roho katika kuhisi neema na adhabu kwenye kaburi? Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema baada ya kuulizwa swali hili yafuatayo:

“Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamekubaliana juu ya kwamba adhabu na neema inakuwa kwenye roho na kiwiliwili vyote viwili. Roho inaneemeshwa na kuadhibiwa peke yake na inaneemeshwa na kuadhibiwa pamoja na kiwiliwili. Kiwiliwili kinaweza kuhisi neema na adhabu pasi na roho? Ahl-us-Sunnah wal-Hadiyt na wanafalsafa wana maoni mawili yanayojulikana juu ya suala hili. Katika suala hili kuna maoni mengine vilevile yasiyokuwa na nguvu ambayo sio katika maoni ya Ahl-us-Sunnah wal-Hadiyth.

Kuna wanaosema kuwa neema na adhabu inahusiana na roho peke yake pasi na kiwiliwili. Haya yanasemwa na wanafalsafa wanaokanusha kuwa viwiliwili vitafufuliwa. Hawa ni makafiri kwa maafikiano ya waislamu. Wanafalsafa wengi katika Mu´tazilah na wengineo wanaoamini kuwa viwiliwili vitafufuliwa wana maoni haya pia. Lakini wanasema kuwa hayo hayatopitika ndani ya kaburi, isipokuwa ni ule wakati viwiliwili vitapotoka ndani ya makaburi. Wanapinga kuwa viwiliwili ndani ya makaburi ndivyo vitavyoadhibiwa peke yake. Wanaonelea kuwa roho ndizo ima zenye kuneemeshwa au zenye kuadhibiwa ndani ya makaburi. Siku ya Qiyaamah roho na viwiliwili vitaadhibiwa vyote viwili. Baadhi ya makundi ya waislamu katika wanafalsafa wana maoni haya, Ahl-ul-Hadiyth na wengineo. Hili ndio chaguo la Ibn Hazm na Maysara. Maoni haya sio katika yale maoni matatu yasiyokuwa na nguvu. Ni katika maoni ya ambaye anathibitisha adhabu ndani ya kaburi, Qiyaamah na kufufuliwa kwa roho na viwiliwili.

Maoni ya tatu na yasiyokuwa na nguvu ni yale yenye kusema kuwa ndani ya kaburi hakuna kuneemeshwa wala kuadhibiwa mpaka itapofika siku ya Qiyaamah. Haya yanasemwa na Mu´tazilah na wengine wanaopinga adhabu na neema za ndani ya kaburi. Mapote yote haya yamepotea katika suala la kaburi, lakini wako bora kati na kati kuliko wanafalsafa kwa sababu wao wanathibitisha Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 220-221
  • Imechapishwa: 14/12/2016