Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
83 – Kwa sababu kuna sampuli mbili za elimu: elimu inayopatikana kwa viumbe na elimu iliyokosekana kwa viumbe.
MAELEZO
Kuna aina mbili ya elimu: Elimu ambayo Allaah ameificha Kwake mwenyewe na hakuna yeyote anayeijua isipokuwa Yeye tu (Subhaanahu wa Ta´ala) –nayo ni ile elimu ya mambo yaliyofichikana. Elimu nyingine ni ile ilioko kati ya viumbe. Elimu hiyo Allaah ndiye kawafunza nayo kwa sababu ina manufaa na wao. Elimu hiyo Allaah ameiteremsha ndani ya vitabu Vyake na akawatumiliza kwayo Mitume Yake:
رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ
“Ee Mola wetu, wapelekee Mtume atokamana na wao atakayewasomea Aayah Zako na atakayewafunza Kitabu na Hekima.”[1]
Kitabu ni Qur-aan na hekima ni Sunnah. Maoni mengine yanasema ni kuwa na uelewa katika dini ya Allaah. Allaah ametufunza na Mtume Wake pia ametufunza:
كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ
”Kama Tulivyomtuma kwenu Mtume anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayah Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hekima na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua.”[2]
[1]2:129
[2]2:151
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 115
- Imechapishwa: 04/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)