Swali 101: Unasemaje juu ya wanazuoni wa Madiynah wanaolingania katika Salafiyyah? Je, matendo yao ni ya sawa?
Jibu: Mimi sijui kitu kwa wanazuoni wa Madiynah[1] isipokuwa kheri tu. Ninachojua ni kuwa wametaka kuwabainishia watu makosa ambayo baadhi ya watunzi na baadhi ya watu wametumbukia ndani yake, kwa sababu tu wanawatakia watu kheri. Hawajamsemea uwongo yeyote. Wananukuu maneno kwa ukurasa, mjeledi na msitari. Rejeeni katika yale waliyonukuu. Ikiwa wamesema uwongo tubainishieni. Sisi haturidhii uwongo. Rejeeni vitabu vyao walivyovikosoa. Tuleteeni nukuu moja waliyosema uwongo kwayo au wamepindisha. Katika hali hiyo mimi niko pamoja nanyi.
Hata hivyo si sahihi kuwaambia watu wanyamaze, wapuuze batili, wasiraddi na wasibainishe. Huku ni kuificha haki. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ
“Wakati alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu [akawaambia:] “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha!”[2]
إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ
“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja za wazi na mwongozo baada ya kuwa tumeyabainisha kwa watu ndani ya Kitabu, hao anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.”[3]
Tunaona makosa kisha tunyamaze na kuwaacha watu wanatangatanga? Hapana, jambo hilo halijuzu kabisa. Ni wajibu kubainisha haki kutokana na batili. Yule mwenye kuridhia mwache aridhie na yule mwenye kukasirika mwache akasirike.
[1] Wanaokusudiwa ni Muhammad Amaan al-Jaamiy (Rahimahu Allaah), Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, ´Ubayd al-Jaabiriy, ´Aliy al-Faqiyhiy, Swaalih as-Suhaymiy na Muhammad bin Haadiy – Allaah awahifadhi wote. Baada ya fadhilah za Allaah watu hawa ndio ambao wanawafumbua macho wanafunzi wengi kuhusu pote la al-Ikhwaan al-Muslimuun na kuwaraddi viongozi wao.
[2] 3:187
[3] 2:159
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 237-238
- Imechapishwa: 12/08/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
Swali 101: Unasemaje juu ya wanazuoni wa Madiynah wanaolingania katika Salafiyyah? Je, matendo yao ni ya sawa?
Jibu: Mimi sijui kitu kwa wanazuoni wa Madiynah[1] isipokuwa kheri tu. Ninachojua ni kuwa wametaka kuwabainishia watu makosa ambayo baadhi ya watunzi na baadhi ya watu wametumbukia ndani yake, kwa sababu tu wanawatakia watu kheri. Hawajamsemea uwongo yeyote. Wananukuu maneno kwa ukurasa, mjeledi na msitari. Rejeeni katika yale waliyonukuu. Ikiwa wamesema uwongo tubainishieni. Sisi haturidhii uwongo. Rejeeni vitabu vyao walivyovikosoa. Tuleteeni nukuu moja waliyosema uwongo kwayo au wamepindisha. Katika hali hiyo mimi niko pamoja nanyi.
Hata hivyo si sahihi kuwaambia watu wanyamaze, wapuuze batili, wasiraddi na wasibainishe. Huku ni kuificha haki. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ
“Wakati alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu [akawaambia:] “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha!”[2]
إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ
“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja za wazi na mwongozo baada ya kuwa tumeyabainisha kwa watu ndani ya Kitabu, hao anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.”[3]
Tunaona makosa kisha tunyamaze na kuwaacha watu wanatangatanga? Hapana, jambo hilo halijuzu kabisa. Ni wajibu kubainisha haki kutokana na batili. Yule mwenye kuridhia mwache aridhie na yule mwenye kukasirika mwache akasirike.
[1] Wanaokusudiwa ni Muhammad Amaan al-Jaamiy (Rahimahu Allaah), Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, ´Ubayd al-Jaabiriy, ´Aliy al-Faqiyhiy, Swaalih as-Suhaymiy na Muhammad bin Haadiy – Allaah awahifadhi wote. Baada ya fadhilah za Allaah watu hawa ndio ambao wanawafumbua macho wanafunzi wengi kuhusu pote la al-Ikhwaan al-Muslimuun na kuwaraddi viongozi wao.
[2] 3:187
[3] 2:159
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 237-238
Imechapishwa: 12/08/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/101-wanazuoni-wa-madiynah-wanafanya-jambo-la-sawa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)