Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
82 –Haya ni baadhi ya yale ambayo anayahitaji yule ambaye moyo wake umetiwa nuru miongoni mwa wale mawalii wa Allaah (Ta´ala) na ni ngazi ya wale ambao wamebobea katika elimu.
MAELEZO
Wanahitajia mambo haya katika mipango na makadirio ya Allaah. Unatakiwa kuamini makadirio na ngazi zake nne. Unatakiwa pia kuamini upambanuzi wake uliotajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah. Usiingie ndani ya mambo ya mijadala na upinzani. Unachotakiwa ni wewe kufanya matendo mema na sababu zinazofaa.
Ambao wamebobea katika elimu ni wale ambao wana elimu imara na iliyobobea. Hawana mashaka, hawana ujinga. Wanaamini mipango na makadirio ya Allaah, wanatenda matendo mema na kujiepusha na matendo maovu. Hawapekui siri ya Allaah, hawavutani wala kupingana na mambo hayo. Hivo ndivo wanavyokuwa wale ambao wamebobea katika elimu na kuhusu wajinga huingia ndani ya upotofu na mambo mengine waliyoyazua.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 114-115
- Imechapishwa: 04/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)