Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

81 – Yule atakayehoji kuhusu matendo Yake basi amerudisha hukumu ya Kitabu, na yeyote anayerudisha nyuma hukumu ya Kitabu anakuwa miongoni mwa makafiri.

MAELEZO

Bi maana anayehoji ni kwa nini Allaah amefanya hivi na vile, ni kwa nini Allaah amekadiria hivi na vile, amerudisha nyuma hukumu ya Kitabu. Kwa sababu Allaah anasema:

لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ

“Haulizwi kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.”[1]

Yule mwenye kurudisha nyuma hukumu ya Kitabu na Sunnah, akapingana navyo na akaenda katika akili na fikira, anakuwa miongoni mwa makafiri kwa sababu kuamini Qur-aan na Sunnah ni nguzo miongoni mwa nguzo za imani.

[1]21:23

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 04/11/2024