Katika Hadiyth hii kuna hukumu zifuatazo:

1 – Wajibu wa kufunga Ramadhaan.

2 – Kufunga Ramadhaan ni faradhi moja ya miongoni mwa faradhi za Uislamu.

3 – Ni nguzo ya pili kati ya nguzo za Uislamu. Allaah (Ta’ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Enyi mlioamini! Mmeandikiwa [fardhi ya] swawm kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu mpate kumcha.”[1]

Kisha baada ya hapo akasema:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi [mpya] na afunge  swawm.”[2]

Amri hii ni kwa njia ya ulazima. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Uislamu umejengwa juu ya mambo matano: kushuhudia kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji katika Nyumba tukufu ya Allaah.”[3]

[1] 02:183

[2] 02:185

[3] al-Bukhaariy (08) na Muslim (16).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/437-438)
  • Imechapishwa: 23/02/2025