10. Mume kumuosha mke baada ya kufa na kinyume chake

Swali 10: Je, inafaa kwa mwanamke kumuosha mume wake baada ya kufa kwake? Je, inafaa kwa mwanamme kumuosha mke wake baada ya kufa kwake?

Jibu: Dalili za ki-Shari´ah zimefahamisha kwamba hapana vibaya kwa mke kumuosha mume wake na kumwangalia. Kama ambavo hapana vibaya pia kwa mke kumuosha mume wake na kumwangalia. Asmaa´ bint ´Umays (Radhiya Allaahu ´anhaa) alimuosha mume wake Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh). Vilevile Faatwimah aliacha anausia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ndiye amuoshe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 12/12/2021