وأول الرسل نوح عليه السلام، وآخرهم محمد صلى الله عليه وآله وسلم . مما قال تعالى

Mtume wa kwanza ni Nuuh (´alayhis-Salaam). Mtume wa mwisho ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ

“Hakika Tumekufunulia Wahy kama Tulivyomfunulia Wahy Nuuh na Manabii baada yake.”[1]

وقال تعالى

Allaah (Ta´ala) amesema tena:

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ

“Na Muhammad si yeyote isipokuwa ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume.”[2]

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا

“Hakuwa Muhammad baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima kwa kila kitu ni Mjuzi.”[3]

وأفضل الرسل: نبينا محمد  ، وأفضل البشر بعد الأنبياء صلى الله عليهم وسلم: أبو بكر رضي الله عنه ، وعمر رضي الله عنه، وعثمان رضي الله عنه، وعلي رضي الله عنه . ورضي الله عنهم أجمعين

Mtume bora ni Nabii wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Watu bora baada ya Manabii ni Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh), halafu ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh), kisha ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na halafu ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Allaah awawie radhi wote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

وخير القرون قرني ثم الذين يلونهم ثم الذين يلونهم

“Karne bora ni ya kwangu, kisha itayofuatia kisha itayofuatia.”[4]

وعيسى  ينزل من السماء ويقتل الدجال
والحمد لله رب العالمين
تمت على ما تقدم

Vilevile ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atateremka kutoka mbinguni na atamuua ad-Dajjaal[5].

Himdi zote zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu. Mwisho.

[1] 04:163

[2] 03:144

[3] 33:40

[4] al-Bukhaariy (2652) na Muslim (6635)

[5] Muslim (7560).

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 30-32
  • Imechapishwa: 25/03/2017