68 – Haaruun bin ´Abdillaah amenihadithia: Muhammad bin Yaziyd bin Khunays ametuhadithia: Bwana mmoja amesema:
”Siku moja nilipita karibu na Fudhwayl bin ´Iyaadhw akiwa nyuma ya nguzo peke yake. Alikuwa ni rafiki yangu. Basi nikamjia, nikamsalimia na nikaketi kwake. Akasema: “Ee ndugu yangu, nini kimekukalisha kwangu?” Nikasema: “Nimekukuta upo peke yako na hivyo nikatumia fursa ya upweke wako.” Akasema: “Ama kwa hakika lau usingaliketi kwangu basi ingekuwa kheri kwako na kheri kwangu. Basi chagua, ima nisimame niondoke kutoka kwako na hilo, naapa kwa Allaah ni kheri kwako na kheri kwangu, au wewe usimame uniache.” Nikasema: “Bali mimi nitaondoka kwako. Basi naomba unipe wasia ambao Allaah (´Azza wa Jall) ataninufaisha kwao.” Akasema: “Ee mja wa Allaah! Ficha mahali pako, linda ulimi wako na muombe Allaah (´Azza wa Jall) msamaha kwa ajili ya dhambi yako na kwa ajili ya waumini wanaume na waumini wanawake kama Alivyokuamrisha.”
69 – al-Hasan bin ´Ubayd ametuhadithia: Bwana mmoja alimwambia Bishr al-Haarith:
“Niusie.” Akasema: “Ufanye siri utajo wako na kifanye halali chakula chako.”
70 – Ahmad bin Ibraahiym ametuhadithia: ´Abdus-Swamad bin ´Abdil-Waarith ametuhadithia:
”Hawshab alikuwa analia na kusema: “Jina langu limefika msikiti Mkuu.”
71 – Nimefikiwa na kwamba ´Ubayd bin ´Atwaa’ amesimulia kutoka kwa ´Atwaa’ bin Muslim, ambaye nadhani amesema:
”Nilikuwa mimi na Abu Ishaaq usiku mmoja kwa Sufyaan na yeye alikuwa amelala, basi akainua kichwa chake kwa Abu Ishaaq na akasema: “Jihadhari na umaarufu.”
Abu Mushir amesema:
“Kati yako na kuwa miongoni mwa walioangamia hakuna isipokuwa kuwa katika wanaojulikana.”
72 – al-Hasan bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia: Bishr bin al-Haarith (Rahimahu Allaah) amesema:
“Simjui mtu anayependa ajulikane isipokuwa dini yake imekwenda na amefedheheka.”
Ameeleza ya kwamba Bishr bin al-Haarith amesema:
“Hataonja ladha ya Aakhirah mtu anayependa watu wamtambue.”
73 – Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: as-Swalt bin Hakiym amenihadithia: ´Abdullaah bin Marzuuq amenihadithia:
”Nilimtaka ushauri Sufyaan ath-Thawriy na nikasema: “Waonaje nishuke wapi?” Akasema: “Marri-udh-Dhwahraan; mahali ambapo hakuna mtu yeyote anayekujua.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 91-95
- Imechapishwa: 29/01/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 91-95
Imechapishwa: 29/01/2026
https://firqatunnajia.com/10-mahali-ambapo-hakuna-yeyote-anayekujua/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket