10. Maandiko haya yanakabiliwa kwa kujisalimisha na kuyasadikisha

51 – Mapokezi yote utayosikia ambayo hayakufikiwa na akili yako, kwa mfano maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nyoyo za waja ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa rehema (´Azza wa Jall)… “,

“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hushuka katika mbingu ya chini.”,

“Anashuka siku ya ´Arafah.”,

“Kutaendelea kutupwa ndani ya Moto mpaka pale useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Je, hakuna ziada yoyote?”[1]

mpaka al-Jabbaar aweke unyayo Wake – au mguu Wake – juu yake ambapo utasema: “Tosha, tosha.”,

Maneno ya Allaah (Ta´ala) kumwambia mja:

“Ukija Kwangu kwa kutembea, basi Mimi nitakuchapukia.”,

 “Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hushuka siku ya ´Arafah.”,

“Hakika Allaah alimuumba Aadam katika umbile Lake.”,

na:

“Nilimuona Mola Wangu katika umbo zuri kabisa.”,

na mfano wa Hadiyth kama hizi, ni lazima kwako kujisalimisha, kusadikisha, kuegemeza na kuridhia. Usifasiri chochote katika hayo kwa matamanio yako. Hakika kuamini haya ni jambo la wajibu. Yeyote atayefasiri kitu katika haya kwa matamanio yake au akarudisha kitu katika haya, basi huyo ni Jahmiy.

52 – Yeyote mwenye kudai kuwa anamuona Mola Wake duniani, huyo hamwamini Mola Wake (´Azza wa Jall).

53 – Kumfikiria Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ni Bid´ah, kutokana na maneno yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fikirieni uumbaji na wala msimfikirie Allaah.”[2]

Kumfikiria Mola kunafanya kupenyeza mashaka ndani ya moyo.

[1] 50:30

[02] Abush-Shaykh katika “al-´Adhwamah (05) na Abul-Qaasim al-Aswbahaaniy katika “at-Targhiyb” (668-670). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (1788).

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 81-84
  • Imechapishwa: 17/12/2024