10. Kuenea kwa ujumbe wa Muhammad na ulazima wa kumpenda

Ni lazima kuamini kuwa ujumbe wake ni kwa watu wote; kwa majini na watu. Amesema (Ta´ala):

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا

“Na Hatukukutuma isipokuwa kwa watu wote hali ya kuwa ni mbashiriaji na muonyaji.”[1]

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَى عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا

“Amebarikika Yule ambaye ameteremsha Pambanuzi kwa mja Wake ili awe ni muonyaji kwa walimwengu.”[2]

وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

”Wakati Tulipowaelekeza kwako kundi miongoni mwa majini wakisikiliza Qur-aan, walipoihudhuria walisema: “Nyamazeni [msikilize]!” Ilipokwisha [kusomwa], waligeuka kurudi kwa watu wao wakiwaonya. Wakasema: “Enyi qaumu yetu! Hakika sisi tumesikia [kunasomwa] Kitabu kilichoteremsha baada ya Muusa hali ya kuwa kinayasadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza katika haki na katika njia iliyonyooka. Enyi watu wetu! Mwitikieni mlinganiaji wa Allaah na mwaminini hivyo Atakusameheni madhambi yenu na atakukingeni na adhabu iumizayo.”[3]

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا

“Sema: “Nimefunuliwa Wahy ya kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza, wakasema: “Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya kushangaza – inaongoza katik uongofu, hivyo basi tukaiamini na wala hatutomshirikisha Mola wetu na yeyote.”[4]

Ni lazima pia kumpenda Allaah na kumpenda Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Asiyempenda Allaah na Mtume Wake sio muumini. Kukamilika kwa imani ni mtu atangulize mbele mapenzi ya kumpenda Allaah na Mtume Wake kabla ya mapenzi ya wazazi, watoto, nafsi, wake, ndugu, jamaa, mali, biashara na masikini. Mtu akitanguliza chochote katika mambo hayo kabla ya mapenzi ya Allaah na Mtume Wake, basi ameichengua imani na ni mwenye imani dhaifu. Amesema (Ta´ala):

قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَآؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللّهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُواْ حَتَّى يَأْتِيَ اللّهُ بِأَمْرِهِ وَاللّهُ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ

“Sema: “Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake na majumba mnayoridhika nayo –  [ikiwa vyote hivi] ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Mtume Wake na kupambana jihaad katika njia Yake, basi ngojeeni mpaka Allaah alete Amri Yake; hakika Allaah hawaongoi watu mafasiki.”[5]

Imekuja katika Hadiyth:

“Hatoamini mmoja wenu mpaka mimi niwe ni mwenye kupendwa zaidi kwake kuliko baba yake, mtoto wake na watu wote.”[6]

[1] 34:28

[2] 25:01

[3] 46:29-31

[4] 72:01-02

[5] 09:24

[6] al-Bukhaariy (15) na Muslim (44). Maana ya:

”Hatoamini mmoja wenu… ”

Bi maana ile imani ya wajibu. Makusudio ni kule kukamilika kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 22/03/2023