Kwa maana hii Allaah (Subhaanah) akawaeleza wanazuoni kwa khofu na akasema:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika si venginevo wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni.”[1]

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ

“Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika hapana vyenginevyo wanakumbuka wenye akili tu.”[2]

Allaah akawaeleza wanazuoni wa watu wa Kitabu, waliokuwa wakiishi kabla yetu, kwa unyenyekevu na akasema:

قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا

”Sema: ”Iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake wanaposomewa basi wanaporomoka kifudifudi hali ya kusujudu na wanasema: ”Utakasifu ni wa Mola wetu, hakika ahadi ya Mola wetu lazima itimizwe” na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu.”[3]

Akawaelezea (Ta´ala) hali ya kuwasifu wale ambao wakisikia Kitabu cha Allaah kunawapelekea kupata khofu ndani ya nyoyo zao. Amesema (Ta´ala):

فَوَيْلٌ لِّلْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُم مِّن ذِكْرِ اللَّـهِ

”Basi ole wao wenye nyoyo zilizosusuwaa kwa sababu ya kutajwa Allaah.”[4]

Kulainika kwa nyoyo ni kule kuondoka ususuwavu wake kutokana na unyenyekevu unaozuka na upole unaokuwepo ndani yake. Amesema (Ta´ala):

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ

“Je, haujafika wakati kwa walioamini zinyenyekee nyoyo zao kwa ukumbusho wa Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawarefukia muda, halafu zikawa ngumu nyoyo zao – na wengi miongoni mwao wakatumbukia katika madhambi na kuasi?”[5]

Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Ilikuwa ni miaka minne kati ya kusilimu kwetu na kukaripiwa kwa Aayah hiyo.”[6]

Ameipokea Muslim. an-Nasaa´iy amezidisha:

”Hivyo waumini wakaanza kukaripiana.”[7]

Ibn Maajah amepokea kwamba Ibn-uz-Zubayr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Haikuchukua zaidi ya miaka minne tangu waliposilimu mpaka ilipoteremka Aayah hii ambayo Allaah anawakaripia kwayo.”[8]

[1] 35:28

[2] 39:9

[3] 17:107-109

[4] 39:22-23

[5] 57:16

[6] Muslim (3027).

[7] an-Nasaa’iy (11568).

[8] Ibn Maajah (4192).

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 49-52
  • Imechapishwa: 24/11/2025