6- Kujitapikisha. Kujitapikisha kunamfunguza yule mwenye kufunga kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Hapa ni pale ambapo atajitapikisha kwa makusudi. Ama akijizuia na matapishi yakamshinda basi hakumfunguzi mwenye kufunga. Kutokana na yale yaliyopokelewa kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ambaye yatamshinda matapishi basi halazimiki kulipa. Na ambaye atajitapisha basi ni lazima kwake kulipa.”[1]

Ibn Mundhiriy amesema:

“Wanachuoni wameafikiana juu kuharibika swawm ya mwenye kujitapikisha kwa makusudi.”[2]

[1] Abu Daawuud (2380), at-Tirmidhiy (720), Ibn Maajah (1676). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan na al-Haakim.

[2] Tazama ”al-Ijmaa´” (49/126) ya Ibn-ul-Mundhiriy.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 16
  • Imechapishwa: 18/04/2019