Suala hili limejengwa juu ya msingi, nao ni kwamba kuritadi kunabatilisha matendo mara moja au hayabatiliki isipokuwa mpaka mtu aje katika hali hiyo. Katika hili kuna kauli mbili zinazotambulika kwa wanazuoni – na yote mawili yamepokelewa kutoka kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah). Tukisema kuwa kuritadi kunabatilisha matendo mara moja, basi pale mtu anapoingia tena katika Uislamu aanze upya na yanabatilika yale matendo yote aliyoyafanya kabla ya Uislamu. Na tukisema kuwa hayabatiliki isipokuwa akifa katika hali ya kuwa murtadi, basi atakaporudi Uislamu zinarejea thawabu za matendo yake. Vivyo hivyo mja anapofanya tendo jema kisha akafanya tendo ovu linalobatilisha lile jema, kisha akatubia kutokana na hilo tendo ovu, je, humrejea thawabu ya lile tendo jema la awali? Hili linarejea katika msingi huo. Suala hili limekuwa likiniacha na wasiwasi ndani yangu. Nami nimekuwa nikilifuatilia kwa bidii kutaka maoni ya kweli ndani yake wala sijakuta mwenye kunituliza moyo wangu kwa jambo hilo. Jambo linalodhihiri – na Allaah (Ta´ala) ndiye anajua zaidi, Kwake panatafutwa msaada na hapana nguvu wala uwezo isipokuwa kwa msaada Wake – ni kwamba matendo mema na matendo maovu hupingana na kukabiliana na hukumu huenda kwa lililotawala; nalo humshinda linalozidiwa, kiasi kwamba hilo lililozidiwa kama kwamba halikuwepo. Basi pindi matendo mema yakimzidi mja, hayo mema yake mengi huinua na kufuta maovu yake. Na anapotubia tendo ovu, hutokana na tawbah hiyo matendo mema mengi yanayozidi na kuzidiana na lile tendo jema lililoharibika kwa sababu ya lile ovu. Iwapo tawbah imekusudiwa kwa azma ya kweli, ikawa sahihi na kutoka katika moyo wa ndani kabisa, basi huunguza yaliyotangulia miongoni mwa matendo maovu kiasi kwamba ni kama hayakuwapo. Kwani mja anapotubia dhambi basi hana dhambi tena. Hakiym bin Hizaam (Radhiya Allaahu ´anh) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu kuacha huru watumwa, kuunga ukoo na wema alioufanya alipokuwa katika shirki kama mtu hupata thawabu juu yake? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajibu:
“Umeingia Uislamu juu ya mema uliyoyatanguliza.”[1]
Hii inapelekea kwamba Uislamu ulimrudishia thawabu za yale matendo mema yaliyokuwa batili kwa sababu ya shirki. Lakini alipotubia shirki, thawabu za matendo yake ya kale zikamrudia. Hali ni hivyo hivyo kwa mja akitubia tawbah ya kweli, ya dhati na ya ikhlaasw, basi huyateketeza yaliyotangulia ya maovu na humrudishia thawabu za matendo mema yake.
Hili linabainsihwa kwa namna ya kwamba maovu ni kama maradhi ya moyo, kama vile homa, maumivu na magonjwa ya mwili. Mgonjwa anapopona maradhi yake kwa afueni kamili, hurudia nguvu zake au kuzidi hata kuwa kama kwamba hakuwahi kudhoofika kabisa. Basi nguvu za awali ni mfano wa matendo mema, maradhi mfano wa dhambi na afya na uzima mfano wa tawbah. Kama ilivyo kwa mgonjwa ambaye afya yake haiwezi kumrudia kabisa kwa udhaifu wa kinga yake, wapo pia wanaorudia afya yao kama ilivyokuwa kwa sababu ya uwezo wa kinga kupambana na sababu za maradhi na mwili ukarudi kwenye ukamilifu wa awali. Wapo pia wanaorudi wakiwa na afya bora zaidi na nguvu zaidi na uchangamfu mwingi kwa sababu ya nguvu ya sababu za kupona na kuzishinda sababu za udhaifu na maradhi, kiasi kwamba huenda ugonjwa ule ukawa ndio sababu ya afya bora zaidi. Kama asemavyo mshairi:
Huenda lawama yako ikawa na mwisho mwema –
na mara nyingine miili hupata siha kwa maradhi.
Vivyo hivyo mja baada ya tawbah huwa katika daraja hizi tatu. Allaah ndiye Mwenye kuwafikisha. Hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye na wala hapana mola wa haki isipokuwa Yeye.
[1] al-Bukhaariy (1436, 2220 na 2538) na Muslim (123).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 23-25
- Imechapishwa: 30/07/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 23-25
Imechapishwa: 30/07/2025
https://firqatunnajia.com/10-hali-baada-ya-dhambi/