Ahmad (3/502) amesema: Yuunus bin Ahmad ametuhadithia: al-´Attwaaf ametuhadithia: Mujammiy´ bin Ya´quub amenihadithia, kutoka kwa kijana mmoja kutoka Qubaa’, ambaye alikutana na mzee mmoja aliyesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitujia Qubaa´ na akaketi kwenye kivuli cha mwekundu. Watu wakamkusanyikia ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaomba maji, akapewa na akanywa. Nilikuwa nimekaa upande wake wa kulia na mimi nilikuwa mdogo kuliko wengine waliokuwepo. Akanipea bakuli, nikanywa na nikahifadhi kuwa alituswalisha siku hiyo akiwa amevaa viatu vyake – bila kuvivua.”
Ameipokea adh-Dhwiyaa’ (4/221-334), at-Twahaawiy (1/512), ambaye amemtaja Muhammad bin Ismaa´iyl baina ya Mujammiy´ bin Ya´quub na Swahabah, ambaye amemtaja jina kama ´Abdullaah bin Abiy Habiybah, na Ibn Sa´d (1/167 – mswada). al-Haythamiy amesema:
”Ameipokea Ahmad, ambaye amemtaja jina ´Abdullaah bin Abiy Habiybah katika upokezi mwingine, na at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr”. Wanaume wa Ahmad ni wenye kuaminika.”[1]
[1] Majma´-uz-Zawaa-id (2/53).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 12-13
- Imechapishwa: 01/06/2025
Ahmad (3/502) amesema: Yuunus bin Ahmad ametuhadithia: al-´Attwaaf ametuhadithia: Mujammiy´ bin Ya´quub amenihadithia, kutoka kwa kijana mmoja kutoka Qubaa’, ambaye alikutana na mzee mmoja aliyesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitujia Qubaa´ na akaketi kwenye kivuli cha mwekundu. Watu wakamkusanyikia ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaomba maji, akapewa na akanywa. Nilikuwa nimekaa upande wake wa kulia na mimi nilikuwa mdogo kuliko wengine waliokuwepo. Akanipea bakuli, nikanywa na nikahifadhi kuwa alituswalisha siku hiyo akiwa amevaa viatu vyake – bila kuvivua.”
Ameipokea adh-Dhwiyaa’ (4/221-334), at-Twahaawiy (1/512), ambaye amemtaja Muhammad bin Ismaa´iyl baina ya Mujammiy´ bin Ya´quub na Swahabah, ambaye amemtaja jina kama ´Abdullaah bin Abiy Habiybah, na Ibn Sa´d (1/167 – mswada). al-Haythamiy amesema:
”Ameipokea Ahmad, ambaye amemtaja jina ´Abdullaah bin Abiy Habiybah katika upokezi mwingine, na at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr”. Wanaume wa Ahmad ni wenye kuaminika.”[1]
[1] Majma´-uz-Zawaa-id (2/53).
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 12-13
Imechapishwa: 01/06/2025
https://firqatunnajia.com/10-hadiyth-nikahifadhi-kuwa-alituswalisha-siku-hiyo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket