36 – ´Abdul-Kariym bin Hawzaan ametukhabarisha: Nimemsikia Muhammad bin al-Husayn as-Sulamiy: Nimemsikia Abu Naswr al-Aswbahaaniy: Nimemsikia Muhammad bin ´Iysaa: Abu Sa´iyd al-Kharraaz amesema:
”Elimu ni ile inayokufanya ukatenda na yakini ni ile inayokubeba.”
37 – Muhammad bin ´Ubaydillaah al-Hinnaa-iy ametukhabarisha: Ja´far bin Muhammad bin Nuswayr al-Khuldiy ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin Masruuq ametuhadithia: Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Sa´iyd bin ´Aamir ametuhadithia: Swaalih bin Rustum ametuhadithia: Abu Qilaabah alinambia:
”Allaah akikupa elimu, basi nawe mpe ´ibaadah. Isiwe hamu yako kubwa ni kuwasimulia tu nayo watu.”
38 – Muhammad bin al-Husayn bin al-Fadhwl al-Qattwaan ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ja´far bin Darastuuyah ametukhabarisha: Ya´quub bin Sufyaan ametuhadithia: Abu Bishr, yaani Bakr bin Khalaf, amenihadithia: Sa´iyd bin ´Aamir ametuhadithia: Swaalih bin Rustum ametuhadithia: Abu Qilaabah alinambia:
”Allaah akikupa elimu, basi nawe mpe ´ibaadah. Isiwe hamu yako kubwa ni kuwasimulia tu nayo watu.”
39 – Abul-Hasan Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz bin Ja´far al-Bardha´iy ametukhabarisha: Ahmad bin Muhammad bin ´Imraan ametukhabarisha: Ahmad bin al-Qaasim bin Naswr ametuhadithia: Muhammad bin Sulaymaan bin Habiyb Luwayn ametuhadithia: Abu Muhammad al-Atrabulusiy amenihadithia, kutoka kwa Abu Ma´mar, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:
”Hamu kubwa ya wanazuoni ni kuzingatia ilihali hamu kubwa ya wapumbavu ni kusimulia.”
40 – Abul-Faraj ´Abdul-Wahhaab bin ´Abdil-´Aziyz bin al-Haarith bin Asad bin al-Layth bin Sulaymaan bin al-Aswad bin Sufyaan bin Yaziyd bin Ukaynah bin ´Abdillaah at-Tamiymiy ametukhabarisha kutoka kwa hifdhi yake: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia ´Aliy bin Abiy Twaalib akisema:
”Elimu inayaita matendo; ima ikayaitikia na vinginevyo inaondoka.”
Alihesabu baba tisa.
41 – al-Qaadhwiy Abul-Qaasim ´Aliy bin al-Muhsin bin ´Aliy bin Muhammad bin Abiyl-Fahm at-Tannuukhiy ametukhabarisha: Nilipata kwenye kitabu cha baba yangu: Ahmad bin Abiyl-´Alaa’ al-Makkiy amenihadithia: Ishaaq bin Muhammad bin Abaan an-Nakha´iy ametuhadithia: an-Nawfaliy amenihadithia, kutoka kwa al-Haarith bin ´Ubaydillaah: Nimemsikia Ibn Abiy Dhi’b akisimulia kutoka kwa Ibn-ul-Munkadir:
”Elimu inayaita matendo; ima ikayaitikia na vinginevyo inaondoka.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 34-36
- Imechapishwa: 12/05/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)