17 – Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba kuna bedui alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Nifunze maneno nitakayosema.” Akamwambia: “Sema:

لاَ إله إلاَّ اللَّه وحدَهُ لا شرِيكَ لهُ، اللَّه أَكْبَرُ كَبِيرًا، والحمْدُ للَّهِ كَثيرًا، وسُبْحانَ اللَّه ربِّ العالمِينَ، وَلاَ حوْل وَلا قُوَّةَ إلاَّ باللَّهِ العَزيز الحكيمِ

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika. Allaah ni mkubwa na mtukufu, himdi zote njema ni za Allaah nyingi, Allaah ametakasika, Mola wa walimwengu. Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah, Mwenye nguvu Aliyeshinda, Mwenye hekima.”

Bedui yule akasema:

“Haya ni kwa ajili ya Mola wangu. Yako wapi yangu?” Akamwambia: “Sema:

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وارْحمني. واهْدِني، وارْزُقْني

“Ee Allaah! Nisamehe, nihurumie, niongoze na uniruzuku.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hii imekusanya aina mbalimbali ya dhikr. Ndani yake kuna ya kwamba bedui ameifanya sehemu mbili; ambazo zote ni kwa ajili ya Allaah. Dhikr ni du´aa yenye kuenea. Alichokusudia bedui ni du´aa kwa ajili yake mwenyewe.

[1] Muslim (2696).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 30/09/2025