Watu wengi hawaujui mwezi huu isipokuwa kuwa ni mwezi wa kubadilisha vyakula na vinywaji. Kwa hiyo wakazidisha kuyapa matamanio ya nafsi zao na wakawa wanazidisha kununua vya ziada vya vyakula na vinywaji. Ni jambo linalotambulika kuwa kuzidisha kula na kunywa husababisha uvivu katika utiifu. Kinachotakiwa kwa muislamu ni kupunguza chakula na kinywaji ili awe na uchangamfu katika utiifu.
Miongoni mwa watu wapo wanaoujua mwezi wa Ramadhaan kuwa ni mwezi wa kulala mchana na kukesha usiku katika yasiyo na manufaa au yenye madhara. Huchangamka usiku mwingi au wote, kisha hulala mchana mpaka wanakosa hata swalah za faradhi. Matokeo yake hawaswali kwa jamaa wala kwa nyakati zake.
Kundi jingine hukaa mezani wakati wa kufuturu na kuacha swalah ya Maghrib kwa mkusanyiko. Makundi haya hayajui thamani ya Ramadhaan wala hayajizuizi kuivunja heshima yake kwa kukesha katika yaliyo haramu, kuacha wajibu na kufanya yaliyoharamishwa.
Sambamba na hao wapo watu wanaoujua mwezi wa Ramadhaan kuwa ni msimu wa biashara na wa kuonesha bidhaa na kutafuta dunia ya haraka. Huchangamka kwa kuuza na kununua na hivyo wakakaa sokoni na kuyahama misikiti. Wakienda misikitini huenda kwa haraka na kwa uzito na hawatulizani humo, kwa sababu utulivu wa macho yao uko masokoni.
Kundi jingine la watu hawaujui mwezi wa Ramadhaan isipokuwa kuwa ni wakati wa kuombaomba misikitini na mitaani. Matokeo yake hutumia muda wao mwingi kwa kwenda na kurudi, kuzunguka huku na huko na kusafiri kutoka mji hadi mji kukusanya mali kwa njia ya kuomba na huku akijionesha kuwa ni mhitaji ilihali ni tajiri, au kujionesha kuwa ana maradhi mwilini ilihali ni mzima. Anaikanusha neema ya Allaah juu yake ya utajiri na afya, anachukua mali isiyo haki yake na anapoteza muda wake wa thamani katika yaliyo madhara kwake. Kwa makundi haya ni nini kilichobaki cha fadhilah ya Ramadhaan?
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 18
- Imechapishwa: 28/01/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 18
Imechapishwa: 28/01/2026
https://firqatunnajia.com/10-aina-mbalimbali-ya-watu-wanavyoipokea-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket