Mlango wa kwanza: Kuhusu hukumu za twahara na maji. Ndani yake kuna masuala mengi:

Suala la kwanza: Maana ya twahara, ubainifu wa umuhimu wake na vigawanyo vyake.

Ndani yake kuna masuala mengi:

Suala la kwanza: Maana ya twahara, ubainifu wa umuhimu wake na vigawanyo vyake.

1-  Umuhimu wa twahara na vigawanyo vyake

Twahara ndio ufunguo wa swalah na ndio sharti ya swalah yenye ukokotezo mkubwa. Ni lazima sharti ikitangulie kile kilichotiliwa sharti.

Twahara imegawanyika aina mbili:

Ya kwanza: Twahara ya kimaana. Nako ni kule mtu kuusafisha moyo wake kutokamana na shirki, maasi na kila kinachoufanya kuwa  mchafi.

Hiyo ndio twahara muhimu zaidi kuliko twahara ya kimwili. Twahara ya kimwili haihakikishwi muda wa kuwa mtu ana najisi ya shirki. Amesema (Ta´ala):

إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ

“Hakika washirikiana ni najisi.”[1]

Ya pili: Twahara ya kuhisiwa. Tutalipambanua katika misitari inayofuata.

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 1
  • Imechapishwa: 06/02/2020