Katika Qur-aan tukufu utaona jinsi Allaah (Ta´ala) amevyobainisha misingi ya dini na tanzu zake. Amebainisha Tawhiyd kwa aina zake zote, bali amebainisha hata adabu za vikao na kuomba idhini. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا فِي الْمَجَالِسِ فَافْسَحُوا يَفْسَحِ اللَّـهُ لَكُمْ ۖ وَإِذَا قِيلَ انشُزُوا فَانشُزُوا
“Enyi mlioamini! Mnapoambiwa: “Fanyeni nafasi katika vikao!” – basi [sogeeni] mfanye nafasi; Allaah atakufanyieni nafasi. Na mnapoambiwa: “Inukeni!” – basi inukeni.”[1]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَىٰ أَهْلِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ فَإِن لَّمْ تَجِدُوا فِيهَا أَحَدًا فَلَا تَدْخُلُوهَا حَتَّىٰ يُؤْذَنَ لَكُمْ ۖ وَإِن قِيلَ لَكُمُ ارْجِعُوا فَارْجِعُوا ۖ هُوَ أَزْكَىٰ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ
”Enyi mloamini! Msiingie nyumba zisizokuwa nyumba zenu mpaka mjitambulishe na muwatolee salamu watu wake. Hivyo ni bora kwenu huenda mkakumbuka. Na msipokuta humo [mtu] yeyote, basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa: “Rejeeni! – basi rejeeni. Huo ni utakaso zaidi kwenu. Na Allaah kwa myatendayo ni Mjuzi.”[2]
Hata adabu za mavazi zimeletwa. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَالْقَوَاعِدُ مِنَ النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَاتٍ بِزِينَةٍ ۖ وَأَن يَسْتَعْفِفْنَ خَيْرٌ لَّهُنَّ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Na wanawake, ambao wamekoma hedhi na wasiyotaraji kuolewa, basi hakuna ubaya juu yao kupunguza baadhi ya nguo zao bila ya kuonyesha mapambo yao [au kujishaua]. Na kama wakijisitiri [kwa kujifunika vyema] ni kheri kwao. Na Allaah ni Mwenye kusikia yote daima, Mjuzi wa yote daima.”[3]
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا
“Ee Nabii! Waambie wake zako na wasichana zako na wanawake wa waumini wajiteremshie juu yao shungi zao – hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane ili wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[4]
وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ
”Na wala wasipige miguu yao yajulikane yale wanayoyaficha katika mapambo yao.”[5]
وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ
“Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kwa mwenye kumcha Allaah. Na ingieni nyumba zenu kupitia milango yake. Na mcheni Allaah.”[6]
Kuna Aayah zingine nyingi zenye kubainisha kuwa dini hii ni kamilifu. Haihitaji nyongeza yoyote kama ambavo pia haijuzu pia kupunguza chochote. Kwa ajili hii ndio maana Allaah (Ta´ala) amesema pindi alipokuwa akiisifu Qur-aan:
وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ
“Na Tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu.”[7]
Hakuna kitu ambacho watu wanakihitajia katika maisha haya na maisha ya Aakhirah isipokuwa Allaah (Ta´ala) amekibainisha katika Kitabu Chake kwa njia moja au nyingine; kimatamshi, kiashirio, kwa njia ya moja kwa moja na njia isiyokuwa ya moja kwa moja.
[1] 58:11
[2] 24:27-28
[3] 24:60
[4] 33:59
[5] 24:31
[6] 02:189
[7] 16:89
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ibdaa´ fiy Kamaal-ish-Shar´ wa Khatwar-il-Ibtidaa´, uk. 2-3
- Imechapishwa: 23/10/2016

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ibdaa´ fiy Kamaal-ish-Shar´ wa Khatwar-il-Ibtidaa´, uk. 2-3
Imechapishwa: 23/10/2016
https://firqatunnajia.com/1-uislamu-ni-dini-iliyokamilika-na-timilifu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)