Msaada unaombwa kutoka kwa Allaah. Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Himdi zote njema anastahiki Allaah, ambaye anaunga nyoyo zilizovunjika kwa ajili Yake na kutokana na fadhilah Zake anasamehe wale wenye kumuomba msamaha. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee  hana mshirika na hakuna yeyote mfano Wake, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Allaah amemtumiliza kwa uongofu na kwa dini ya haki, ili izishinde dini nyengine zote, na akampa chaguo kati ya kuwa mfalme na Mtume au mja na Mtume. Hivyo akachagua utumwa na ujumbe. Alikuwa akisema:

”Ee Allaah! Nipe uhai nikiwa masikini na unifishe masikini na unikusanye katika mkusanyiko wa masikini.”[1]

Akiashiria utukufu wa hali na ubora wake. Swalah na amani ziwe juu yake, jamaa zake, Maswahabah zake na wale watakaoshikamana na kamba yake.

Ndani ya Kitabu Chake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewasifu wale watu wenye kumnyenyekea na wale wenye kujivunjavunja kutokana na utukufu Wake. Allaah (Ta´ala) amesema:

كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

“… walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.”[2]

إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا

”Hakika waislamu wanaume na wanawake na waumini wanaume na wanawake na watiifu wanaume na wanawake na wasemao ukweli wanaume na wanawake na wanaosubiri wanaume na wanawake na wanyenyekevu wanaume na wanawake na wenye kutoa swadaqah wanaume na wanawake na wafungao swawm wanaume na wanawake na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake na wanaomtaja Allaah kwa wingi wanaume na wanawake – Allaah amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.”[3]

Amewaeleza waumini kwamba ni wenye kumnyenyekea katika ´ibaadah yao tukufu zaidi ambayo wanaihifadhi:

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ

“Hakika wamefaulu waumini; ambao katika swalah zao ni wenye kunyenyekea.”[4]

قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا

”Sema: ”Iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake wanaposomewa basi wanaporomoka kifudifudi hali ya kusujudu na wanasema: ”Utakasifu ni wa Mola wetu, hakika ahadi ya Mola wetu lazima itimizwe” na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu.”[5]

[1] at-Tirmidhiy (2352). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2352).

[2] 21:90

[3] 33:35

[4] 23:01-02

[5] 17:107-109

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 27-29
  • Imechapishwa: 24/11/2025