09 – Ole ole swalah
Ee kijakazi wa Allaah! Ichunge swalah ndani ya wakati wake na itekeleze kwa njia inayokubalika katika Shari´ah pamoja na nguzo, sharti zake, maneno na vitendo vyake vinavyopendeza. Usiicheleweshe swalah nje ya wakati wake. Kumepokelewa makemeo makali kwa ambaye anaichelewesha swalah nje ya wakati wake bila ya udhuru unaokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Amesema (Ta´ala):
فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ
“Ole wao waswaliji, ambao wanapuuza swalah zao.”[1]
Isitoshe unaposwali basi uhudhurishe moyo wako. Tambua ya kwamba umesimama mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hivyo basi, jihadhari na kuidonoa swalah yako kama anavyodonoa kunguru. Hivi ndivo wanavofanya baadhi ya wasichana – Allaah awaongoze. Ni kana kwamba wanataka kujikwamua kutokamana na swalah. Je, hutambui ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kitulizo cha jicho langu kimefanywa ni ndani ya swalah.”[2]
Je, hutambui ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tupe raha kwa swalah, ee Bilaal.”
Ameipokea Ahmad.
Hali ya baadhi ya wasichana inasema:
”Tupe raha kutokamana na swalah!”
Kwa hivyo, mche Allaah, ee mjakazi wa Allaah! Jua ya kwamba jambo la kwanza utakaloulizwa ni Allaah. Ikitengemaa yatatengemaa matendo yaliyosalia na ikiharibika yataharibika matendo yaliyosalia
[1] 107:04-05
[2] Ibn Hajar amesema:
”Ameipokea an-Nasaa´iy na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.” (Fath 11/345)
- Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 17-18
- Imechapishwa: 10/02/2026
09 – Ole ole swalah
Ee kijakazi wa Allaah! Ichunge swalah ndani ya wakati wake na itekeleze kwa njia inayokubalika katika Shari´ah pamoja na nguzo, sharti zake, maneno na vitendo vyake vinavyopendeza. Usiicheleweshe swalah nje ya wakati wake. Kumepokelewa makemeo makali kwa ambaye anaichelewesha swalah nje ya wakati wake bila ya udhuru unaokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Amesema (Ta´ala):
فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ
“Ole wao waswaliji, ambao wanapuuza swalah zao.”[1]
Isitoshe unaposwali basi uhudhurishe moyo wako. Tambua ya kwamba umesimama mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hivyo basi, jihadhari na kuidonoa swalah yako kama anavyodonoa kunguru. Hivi ndivo wanavofanya baadhi ya wasichana – Allaah awaongoze. Ni kana kwamba wanataka kujikwamua kutokamana na swalah. Je, hutambui ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kitulizo cha jicho langu kimefanywa ni ndani ya swalah.”[2]
Je, hutambui ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tupe raha kwa swalah, ee Bilaal.”
Ameipokea Ahmad.
Hali ya baadhi ya wasichana inasema:
”Tupe raha kutokamana na swalah!”
Kwa hivyo, mche Allaah, ee mjakazi wa Allaah! Jua ya kwamba jambo la kwanza utakaloulizwa ni Allaah. Ikitengemaa yatatengemaa matendo yaliyosalia na ikiharibika yataharibika matendo yaliyosalia
[1] 107:04-05
[2] Ibn Hajar amesema:
”Ameipokea an-Nasaa´iy na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.” (Fath 11/345)
Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 17-18
Imechapishwa: 10/02/2026
https://firqatunnajia.com/09-swalah/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket