5 – Mshahara wa mke

Ikiwa mke yuko na mshahara, jambo ambalo linatokezea wakati wa sasa. Mke akiwa ni daktari, mwalimu au mfanya kazi, basi mshahara huo huwasukuma baadhi yao – na pengine wakawa ndio wengi – kubaki bila ya waume, tabu, kutengana na matatizo katika maisha ya ndoa. Mume wake anataka sehemu kutoka katika mshahara huo, vivyo hivyo mama yake, vivyo hivyo baba yake na yeye mwenyewe anahitaji mshahara wake. Matokeo yake mshahara huo unakuwa ni moto kwa mwanamke huyo na kwa familia yake. Nakusudia inakuwa ni moto juu ya mahusiano yake ya kindoa. Kila mmoja anaitazama dunia na hivyo yanaharibika maisha ya kindoa kwa sababu ya pesa hizi. Hali hii inatokea katika jamii yetu.

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 02/04/2024