Smith akanambia: “Wewe ni muislamu?” Nikasema: “Ndio.” Akasema: “Muhammad alikuwa hajui historia.” Nikamwambia: “Umejuaje?” Akajibu: “Amesema katika Qur-aan:

يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا

“Ee dada wa Haaruun! Hakuwa baba yako mtu muovu na wala mama yako hakuwa kahaba.” (19:28)

Nikamwambia: “Inapokuja katika elimu kuhusu njama za wakristo na uadui wao dhidi ya Uislamu, basi wewe humfikii George Sale[1] ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kutafsiri Qur-aan tukufu kwa kingereza. Alisema kwenye maelezo yake ya chini kuhusu hiyo Aya:

“Pingamizi ya wakuu wetu wa kikristo juu ya yaliyokuja katika Aya hii si ya sawa. Hakuna mwanachuoni yeyote wa Kiislamu aliyesema kuwa Haaruun huyu ni nduguye Muusa mpaka isemwe ya kwamba kulikuwa karne nyingi kati ya Muusa na nduguye Haaruun na ´Iysaa na mamake.”

Akasema: “Ahmad Khaan, ambaye ni mwanzilishi wa AMU[2], alikubaliana na pingamizi hii.” Nikasema: “Mimi simtambui Ahmad Khaan wala sijui ni nani. Mimi nimekwambia tu jawabu la yaliyosemwa na mmoja katika watangulizi wenu aliye na uadui juu ya Uislamu. Huna lolote la kusema.”

[1] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/George_Sale

[2] Tazama http://www.amu.ac.in/

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 26
  • Imechapishwa: 16/10/2016