Kuamini siku ya Mwisho ina maana ya kusadikisha yale yote yatayokuwa baada ya mauti katika yale aliyoeleza Allaah na Mtume Wake kukiwemo adhabu na neema zilizomo ndani ya kaburi, kufufuliwa kutoka ndani ya makaburi, kukusanywa kiwanjani, kufanyiwa hesabu, kupimwa kwa matendo, kupewa madaftari kwa mkono wa kulia au mkono wa kushoto, Njia, Pepo, Moto, kujiandaa juu ya mambo hayo kwa njia ya kufanya matendo mema, kuacha matendo maovu na kutubu kwayo.

Watu wenye kuamini mazingira na washirikina wameikufuru siku ya Mwisho. Vilevile mayahudi na manaswara hawakuiamini imani sahihi na inayotakikana ijapo watakuwa wanaamini kuwa itatokea:

وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ

“Wakasema: “Hatoingia Peponi isipokuwa aliyekuwa myahudi au mnaswara.””[1]

قَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ

“Wamesema: “Hautatugusa Moto isipokuwa siku chache za kuhesabika.””[2]

[1] 02:111

[2] 03:24

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Usuwl ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 22
  • Imechapishwa: 12/05/2022