39 – Anas  (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiseme mmoja wenu: “Ee Allaah! Nisamehe Ukitaka! Ee Allaah! Nirehemu Ukitaka!” Akate azimio la maombi. Kwani Allaah hakuna amtenzaye nguvu.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

2- Kwa Muslim imekuja kwa tamko lisemalo:

“Anatakiwa aifanye kubwa shauku yake. Kwani Allaah hakioni kikubwa kwa kile alichokitoa.”

MAELEZO

Hadiyth hii inafahamisha makatazo ya kubagua katika kuomba du´aa. Asiseme:

“Ee Allaah! Nisamehe ukitaka.”

Bali ni wajibu kwake kukata azimio la maombi, kwani kufanya ubaguzi kunajulisha kutokuwa na shauku ya kile kinachoombwa na kwamba akipata amepata na asipopata hana haja. Bali afanye azimio katika maombi, kwa sababu Allaah hakuna wa kumtenza nguvu na wala hakioni kikubwa kile alichokitoa. Hazina Yake imejaa.

[1] al-Bukhaariy (6338) na Muslim (2678).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 44
  • Imechapishwa: 12/10/2025