Madhambi yanafupisha umri wa kuishi na ni jambo lisiloepukika kwamba yanayokomeza baraka zake. Kama ambavyo uchaji unarefusha umri wa kuishi, basi madhambi yanafupisha umri wa kuishi. Wanachuoni wametofautiana juu ya suala hili. Kuna waliosema kuwa umri wa mtenda dhambi kufupika maana yake ni kwamba baraka katika umri wake inaondoka na kupotea. Hili ni kweli na ni moja katika madhara ya maasi. Wengine wakasema umri wa kuishi kwake unapungua kikweli kama inavyopungua riziki.

Kwa ujumla ni kwamba pindi mtenda madhambi anapompa mgongo Allaah na kujishughulisha na madhambi basi yanateketea masiku ya uhai wake. Haya atayapata ile siku atakayosema:

يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي

“Atasema: “Ee, laiti ningelitanguliza [matendo mazuri] kwa ajili ya uhai wangu [wa Aakhirah].”[1]

[1] 89:24

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 67
  • Imechapishwa: 05/01/2018