45 – Unafiki ni kule mtu kudhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri.
46 – Tambua kuwa dunia ni ulimwengu wa imani na Uislamu.
47 – Kati ya ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuna waumini inapokuja katika hukumu zao, mirathi yao, vichinjwa vyao pamoja haki ya kuwaswalia.
48 – Hatumshuhudilii yeyote kuwa na imani kamilifu mpaka atekeleze Shari´ah zote za Kiislamu. Endapo atapuuzia kitu katika hayo, anazingatiwa kuwa na imani pungufu mpaka atubie. Tambua kuwa imani yake inaegemezwa kwa Allaah (Ta´ala), sawa iwe ni imani kamilifu au pungufu – isipokuwa akidhihirisha kwako kupuuzia Shari´ah za Kiislamu.
49 – Ni Sunnah kuwaswalia waislamu wenye kufa. Waliopigwa mawe, wazinifu wanaume na wazinifu wanawake, wenye kujiua na waislamu wengine. Hali kadhalika walevi na wengineo. Ni Sunnah kuwaswalia.
50 – Hakuna muislamu yeyote anayetoka katika Uislamu mpaka arudishe nyuma Aayah kutoka katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) au kitu kutoka katika mapokezi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akachinja kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah au akaswali kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Atapofanya kitu katika hayo, basi itakuwajibikia kumtoa katika Uislamu. Asipofanya kitu katika hayo, basi ni muumini muislamu kwa jina, na si kwa uhakika.
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 80-81
- Imechapishwa: 17/12/2024
45 – Unafiki ni kule mtu kudhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri.
46 – Tambua kuwa dunia ni ulimwengu wa imani na Uislamu.
47 – Kati ya ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuna waumini inapokuja katika hukumu zao, mirathi yao, vichinjwa vyao pamoja haki ya kuwaswalia.
48 – Hatumshuhudilii yeyote kuwa na imani kamilifu mpaka atekeleze Shari´ah zote za Kiislamu. Endapo atapuuzia kitu katika hayo, anazingatiwa kuwa na imani pungufu mpaka atubie. Tambua kuwa imani yake inaegemezwa kwa Allaah (Ta´ala), sawa iwe ni imani kamilifu au pungufu – isipokuwa akidhihirisha kwako kupuuzia Shari´ah za Kiislamu.
49 – Ni Sunnah kuwaswalia waislamu wenye kufa. Waliopigwa mawe, wazinifu wanaume na wazinifu wanawake, wenye kujiua na waislamu wengine. Hali kadhalika walevi na wengineo. Ni Sunnah kuwaswalia.
50 – Hakuna muislamu yeyote anayetoka katika Uislamu mpaka arudishe nyuma Aayah kutoka katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) au kitu kutoka katika mapokezi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akachinja kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah au akaswali kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Atapofanya kitu katika hayo, basi itakuwajibikia kumtoa katika Uislamu. Asipofanya kitu katika hayo, basi ni muumini muislamu kwa jina, na si kwa uhakika.
Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 80-81
Imechapishwa: 17/12/2024
https://firqatunnajia.com/09-kuwaswalia-swalah-ya-jeneza-waislamu-waliokufa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)