16 – Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:
“Kila kiungo cha mwili wa mmoja wenu kinapambaukiwa kutoa swadaqah. Kila Tasbiyh ni swadaqah, kila Tahmiyd ni swadaqah, kila Tahliyl ni swadaqah, kila Takbiyr ni swadaqah, kuamrisha mema ni swadaqah na kukataza maovu ni swadaqah. Zinamtosheleza kutokana na hayo Rak´ah mbili anazorukuu za Dhuhaa.”[1]
MAELEZO
Hadiyth mbili zinafahamisha kuwa kila Tashiyh ni swadaqah, kila Tahmiyd ni swadaqah, kila Tahliyl ni swadaqah na kila Takbiyr ni swadaqah.
Hadiyth hii inafahamisha kuwa mwanadamu anatakiwa kuvitekelezea wajibu viungo vyake vya mwili.
Dhikr hii, katika Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl na Takbiyr, ndio swadaqah ya viungo hivi. Vivyo hivyo Rak´ah mbili za Dhuhaa zinasimama mahali pa dhikr hizo, kwa imekusanya aina mbalimbali ya dhikr za kimoyo, kimaneno na kivitendo. Jengine swalah ndio kitendo kinachopendeza zaidi kwa Allaah.
Dhuhaa wakati wake unaanza pale ambapo jua linachomoza kiasi cha mkuki mpaka punde kidogo kabla ya kupinduka kwake.
[1] Muslim (720).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 22-23
- Imechapishwa: 30/09/2025
16 – Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:
“Kila kiungo cha mwili wa mmoja wenu kinapambaukiwa kutoa swadaqah. Kila Tasbiyh ni swadaqah, kila Tahmiyd ni swadaqah, kila Tahliyl ni swadaqah, kila Takbiyr ni swadaqah, kuamrisha mema ni swadaqah na kukataza maovu ni swadaqah. Zinamtosheleza kutokana na hayo Rak´ah mbili anazorukuu za Dhuhaa.”[1]
MAELEZO
Hadiyth mbili zinafahamisha kuwa kila Tashiyh ni swadaqah, kila Tahmiyd ni swadaqah, kila Tahliyl ni swadaqah na kila Takbiyr ni swadaqah.
Hadiyth hii inafahamisha kuwa mwanadamu anatakiwa kuvitekelezea wajibu viungo vyake vya mwili.
Dhikr hii, katika Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl na Takbiyr, ndio swadaqah ya viungo hivi. Vivyo hivyo Rak´ah mbili za Dhuhaa zinasimama mahali pa dhikr hizo, kwa imekusanya aina mbalimbali ya dhikr za kimoyo, kimaneno na kivitendo. Jengine swalah ndio kitendo kinachopendeza zaidi kwa Allaah.
Dhuhaa wakati wake unaanza pale ambapo jua linachomoza kiasi cha mkuki mpaka punde kidogo kabla ya kupinduka kwake.
[1] Muslim (720).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 22-23
Imechapishwa: 30/09/2025
https://firqatunnajia.com/09-kuvitolea-viungo-vya-mwili-swadaqah-kwa-dhikr/