Watu wengi hawana khabari kabisa juu ya maovu yanayobatilisha mema yao. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ
“Enyi walioamini! Msizinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Mtume na wala msiseme naye kwa sauti ya juu kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu, yasije yakaporomoka matendo yenu nanyi hamhisi.”[1]
Basi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewaonya waumini dhidi ya kubatilika kwa matendo yao kwa kumsemesha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sauti ya juu kama wanavyosemezana wao kwa wao. Huku sio kuritadi, bali ni maasi yanayobatilisha matendo na mwenye kuifanya hajihisi nayo. Basi mnamwonaji mtu ambaye msingi wa msimamo wake dhidi ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mwongozo wake na njia yake ni maneno ya mwingine, mwongozo wake na njia yake? Je, huyu si yameharibiwa matendo yake pasi na yeye kuhisi? Miongoni mwa haya ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anayeacha swalah ya ´Aswr basi matendo yake yameharibika.”[2]
Miongoni mwa haya ni maneno yake ´Aaishah kwa Zayd bin Arqam (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alipouza kwa njia fulani ya ribaa:
“Hakika amebatilisha jihaad yake pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), isipokuwa atubie.”[3]
Uuzaji wa biashara wa sura hiyo sio kuritadi, bali kilele chake ni kuwa ni maasi. Basi kujua yale yanayoharibu matendo wakati wa kuitenda na kuyabatilisha au kuipoteza baada ya kutendeka ni miongoni mwa mambo muhimu sana ambayo ni lazima mja ayachunguze, ajilinde juu ya matendo yake na aihadhari. Imekuja katika masimulizi yanayotambulika:
“Hakika mja anaweza kutenda matendo kwa siri, ambayo hajui yeyote isipokuwa Allaah (Ta´ala), kisha akayazungumzia, ikahama kutoka daftari la siri kwenda daftari la wazi, kisha ikawa katika daftari hiyo kulingana na uwazi huo. Na ikiwa ameyazungumza kwa ajili ya kujionyesha, kutafuta hadhi na daraja kwa wasiokuwa Allaah (Ta´ala), basi huyabatilisha kama vile angeyatenda kwa ajili hiyo.”
Je, akitubia, hujerejea kwake thawabu ya matendo hayo? Jawabu ni kwamba ikiwa aliyatenda si kwa ajili ya Allaah (Ta´ala), bali kwa nia hiyo ya kujionyesha, basi hayabadiliki kuwa mema kwa kutubu. Bali faida ya tawbah ni kufuta adhabu tu, basi huwa si yake wala si juu yake.
Ikiwa ameifanya kwa ajili ya Allaah (Ta´ala) kwa imani takasifu, kisha yakamjia ajabu au kujionyesha au akaizungumzia, kisha akatubia kutoka katika hayo na akajutia, basi huu huenda zikarejea thawabu za matendo hayo na yasiharibiwe. Huenda ikasemwa pia kwamba hayarejei kwake, bali aanze matendo upya.
[1] 49:02
[2] al-Bukhaariy (553), an-Nasaa’iy (472) na Ahmad (5/350).
[3] ad-Daaraqutwniy (3/52) na al-Bayhaqiy (5/330-331).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 20-22
- Imechapishwa: 29/07/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 20-22
Imechapishwa: 29/07/2025
https://firqatunnajia.com/09-khatari-ya-mtu-kuzungumzia-matendo-yake-mema/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket