Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Naomba jawabu la kina, Allaah akujaze kheri.

MAELEZO

Muulizaji anamuomba mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) ajibu kwa upambanuzi na asijibu kwa kifupi. Amemtimizia maombi yake na akatoa jawabu la kina mpaka ikawa kitabu hiki kikubwa.

Aidha muulizaji anamuombea Allaah amjaze kheri mtunzi kuwabainishia watu elimu na kuwawekea watu haki wazi. Hapana shaka kuwa kitendo hichi kina malipo makubwa. Jambo hili lina manufaa zaidi kwa watu kuliko swalah zinazopendeza. Kujifunza elimu na kuibainisha elimu kati ya watu ni jambo lina manufaa zaidi kuliko kujishughulisha na ´ibaadah za kujitolea. Kwa sababu elimu yanaenea manufaa yake ilihali ´ibaadah za kujitolea manufaa yake yanakomeka kwa yule mtendaji. Mtu ambaye anaswali usiku mzima au anafunga michana anajinufaisha mwenyewe, na si wengine, ilihali mtu anayetafuta elimu, akafunza, akatoa fatwa na akajibu maswali anawanufaisha wengine vilevile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 33
  • Imechapishwa: 24/07/2024