6 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Zaynab alikuwa akijifakharisha juu ya wakeze Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Familia zenu ndizo zimekuozesheni na mimi nimeozeshwa na Allaah (Ta´ala) kutoka juu ya mbingu ya saba.”

Katika tamko jengine imekuja:

”Allaah ameniozesha mbinguni.”

Katika tamko jengine tena alisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Mwingi wa huruma aliniozesha kwako kutoka juu ya ´Arshi Yake.”

Hadiyth hii ni Swahiyh na ameipokea al-Bukhaariy[1].

[1] Mbili za mwanzo ziko katika ”at-Tawhiyd”. Kadhalika amezipokea pia Ibn Sa´d katika “at-Twabaqaat al-Kubraa” (8/103) na (8/106). at-Tirmidhiy amepokea tamko la kwanza na akasema kuwa ni nzuri na Swahiyh. an-Nasaa’iy (2/76) na Ahmad (3/226) wamepokea hilo tamko la pili, lakini tamko lisemalo “kutoka juu ya mbingu”. Hata hivyo ni moja katika mapokezi ya Ibn Sa´d. Tamko la tatu liko katika mlango wa al-Bukhaariy katika ”at-Tawhiyd”, hilo pia limepokelewa na Anas. Haafidhw Ibn Hajar ameitaja kupitia kwa ash-Sha´biy kwa cheni ya wapokezi inayokosa Swahabah na akasema:

“Ameipokea  at-Twabariy na Abul-Qaasim at-Twahaawiy katika “Kitaab-ul-Hujjah wat-Tibyaan”.” (Fath-ul-Baariy (13/348))

Tamko liliopo kwa at-Twabariy (22/01) liko kwa namna nyingine.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 84
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy