31 – ´Imraan bin al-Huswayn amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia baba yake:

“Ee Huswayn! Unaabudu waungu wangapi?” Akasema: “Saba, sita wako katika ardhi na mmoja Yuko juu mbinguni.” Mtume akamuuliza: “Ni nani unayemwendea wakati wa matumaini na wakati wa khofu?” Huswayn akasema: “Ni Yule ambaye yuko mbinguni.” Mtume akamwambia: “Waache hao sita na mwabudu Yule Aliye mbinguni, na mimi nitakufunza du´aa mbili.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy ambaye amesema kuwa ni nzuri.

32 – ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Warehemu walioko ardhini atakurehemuni Aliyeko juu ya mbingu.” [2]

Ameisahihisha at-Tirmidhiy kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

33 – Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) amesema baada ya kufariki kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yule ambaye alikuwa akimwabudu Muhamamd; basi Muhammad ameshakufa. Na yule ambaye alikuwa akimwabudu Aliye juu ya mbingu; hakika yuhai na hafi.”[3]

Ameipokea ad-Daarimiy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

34 – Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Allaah aliziumba mbingu saba. Akachagua kuishi juu kabisa na akawakaza katika mbingu Zake wale awatakao katika viumbe Wake.”

Muhammad bin Dhakwaan amepwekeka katika kuisimulia kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Ibn ´Umar. Wameipokea kutoka kwake wasimulizi zaidi ya mmoja. Ni maneno ya Mitume na nyumati zilizotangulia.

35 – al-Hasan amesema:

”Yuunus (´alayhis-Salaam) alisikia kusabihi kwa mawe na samaki ambapo na yeye akaanza kusabihi. Akasema katika du´aa yake: ”Ee Bwana Wangu! Makazi Yako ni juu ya mbingu na uwezo Wako uko ardhini.”

Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.

[1] at-Tirmidhiy (3483) ambaye amesema: ”Nzuri na geni.” Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf at-Tirmidhiy”.

[2] al-Albaaniy amesema:

”Ameipokea Abu Daawuud (4941), at-Tirmidhiy (1/350), Ahmad (2/160), al-Humaydiy (591), kupitia kwkae al-Bukhaariy katika ”at-Taariykh” (64/574), Ibn Abiy Shaybah (8/526), al-Haakim (4/159) aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye, al-Khatwiyb katika ”Taariykh Baghdaad” (3/260), al-Bayhaqiy katika ”Shu´b-ul-Iymaan” (7/476) na Abul-Fath al-Khiraqiy katika ”al-Fawaa-id al-Multaqatwah” (222-223) kupitia kwa Sufyaan bin ´Uyaynah, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Abu Qaabuus, mtumwa wa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). at-Tirmidhiy amesema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.” (Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (2/596))

[3] ar-Radd ´alaa Bishr al-Mariysiy, uk. 105.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 56-58
  • Imechapishwa: 02/06/2024