2 – Wanatumia hoja kwa kusema kuwa haya ni matendo yanayofanywa na watu wengi katika miji mingi. Tunajibu hilo kwa kusema kwamba hoja iko katika yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kilichothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kukataza Bid´ah kwa sampuli zake zote ambapo hii ni moja wapo. Matendo ya watu yanapoenda kinyume na dalili hayakutumiwi kama hoja. Haijalishi kitu hata kama yatafanywa kwa wingi:
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ
“Ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, basi watakupoteza na njia ya Allaah.”[1]
Licha ya kwamba katika kila zama bado wanakuwepo watu wenye kukemea Bid´ah hii na kubainisha ubatilifu wake. Hakuna hoja kwa yule mwenye kuendelea kuihuisha baada ya kubainikiwa na haki. Miongoni mwa waliokemea kusherehekea Maulidi katika mnasaba huu ni pamoja na hawa wafuatao:
1 – Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah katika ” Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym”
2 – Imaam ash-Shaatwibiy katika “al-I´tiswaam”
3 – Ibn Haaj katika “al-Madkhal”
4 – Shaykh Taaj-ud-Diyn ´Aliy bin ´Umar al-Lakhmiy ameandika kitabu cha kipekee akikemea maulidi.
5 – Shaykh Muhammad Bashiyr as-Sahsawaaniy al-Hindiy ameyakemea katika kitabu chake “Swiyaanat-ul-Insaan”
6 – Muhammad Rashiyd ar-Ridhwaa ameandika kijitabu cha kipekee kuhusu maulidi.
7 – Shaykh Muhammad bin Ibraahiym Aal as-Shaykh ameandika kijitabu cha kipekee kuhusu maulidi.
8 – Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz
Kuna wengineo mbali na watu hawa bado mpaka hii leo wanaendelea kuandika kukemea Bid´ah hii kila mwaka kwenye magazeti na vipeperushi wakati kunapofanywa Bid´ah hii.
[1] 6:116
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 152
- Imechapishwa: 06/09/2025
2 – Wanatumia hoja kwa kusema kuwa haya ni matendo yanayofanywa na watu wengi katika miji mingi. Tunajibu hilo kwa kusema kwamba hoja iko katika yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kilichothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kukataza Bid´ah kwa sampuli zake zote ambapo hii ni moja wapo. Matendo ya watu yanapoenda kinyume na dalili hayakutumiwi kama hoja. Haijalishi kitu hata kama yatafanywa kwa wingi:
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ
“Ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, basi watakupoteza na njia ya Allaah.”[1]
Licha ya kwamba katika kila zama bado wanakuwepo watu wenye kukemea Bid´ah hii na kubainisha ubatilifu wake. Hakuna hoja kwa yule mwenye kuendelea kuihuisha baada ya kubainikiwa na haki. Miongoni mwa waliokemea kusherehekea Maulidi katika mnasaba huu ni pamoja na hawa wafuatao:
1 – Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah katika ” Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym”
2 – Imaam ash-Shaatwibiy katika “al-I´tiswaam”
3 – Ibn Haaj katika “al-Madkhal”
4 – Shaykh Taaj-ud-Diyn ´Aliy bin ´Umar al-Lakhmiy ameandika kitabu cha kipekee akikemea maulidi.
5 – Shaykh Muhammad Bashiyr as-Sahsawaaniy al-Hindiy ameyakemea katika kitabu chake “Swiyaanat-ul-Insaan”
6 – Muhammad Rashiyd ar-Ridhwaa ameandika kijitabu cha kipekee kuhusu maulidi.
7 – Shaykh Muhammad bin Ibraahiym Aal as-Shaykh ameandika kijitabu cha kipekee kuhusu maulidi.
8 – Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz
Kuna wengineo mbali na watu hawa bado mpaka hii leo wanaendelea kuandika kukemea Bid´ah hii kila mwaka kwenye magazeti na vipeperushi wakati kunapofanywa Bid´ah hii.
[1] 6:116
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 152
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/08-maulidi-yanafanywa-na-watu-wote-ulimwenguni/