52 – Kwa njia hiyohiyo ametuhadithia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa ´Awn, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:
“Ibn Mas´uud alitoka siku moja kutoka nyumbani kwake ambapo watu wakamfuata. Akawageukia na kusema: ”Kwa nini mnanifuata? Naapa kwa Allaah lau mngejua kile ninachojifungia nacho mlango wangu, basi wasingelinifuata hata watu wawili kati yenu.'”
53 – Kwa njia hiyohiyo ametuhadithia Yaziyd bin Haazim, ambaye ameeleza kwamba amemsikia al-Hasan akisema:
“Hakika kelele za viatu nyuma ya mtu ni jambo ambalo mara chache hulisalimisha moyo wa wapumbavu.”
54 – Abu ´Adnaan al-Muqriy ametuhadithia: Yuusuf bin ´Atwiyyah ametuhadithia:
”al-Hasan alitoka siku moja ambapo watu wakamfuata. Akawageukia na kusema: “Mna haja yoyote? Kama hamna, basi jambo hili linaweza kuweka nini katika moyo wa muumini?”
55 – Sablaan ametuhadithia: Dhwamrah ametuhadithia: ´Umar bin ´Abdil-Malik al-Kinaaniy amenihadithia:
”Mtu mmoja alitangamana na Ibn Muḥayriyz safarini. Alipotaka kuagana naye akasema: ”Niusie.” Akasema: “Ukiweza kutojulikana wala usijulikane, ukatembea wala wasitembee kukujia na ukaombwa na wewe usiombe, basi fanya hivyo.”
56 – Ahmad bin Ibraahiym ametuhadithia: Mu’ammil bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Wuhayb bin Khaalid ametuhadithia: al-Jurayriy ametuhadithi: Ayyuub amenambia:
“Ee Abu Mas´uud! Hakika mimi nachelea kwamba ujuzi hautabaki kuwa na matendo mema mbele ya Allaah. Hakika inatokea mimi hupita kwenye vikao, nikawasalimia, lakini sioni kama kuna yeyote anayenifahamu. Wananirudisha salamu halafu wananielekezea swali kana kwamba wote wamenitambua.”
57 – Ahmad ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuub, ambaye amesema:
“Mimi hupita katika kikao, nikawasalimia ambapo wakanirudishia salamu kana kwamba wamenifahamu. Basi kheri gani iliyobaki pamoja na hali kama hii?”
58 – Ahmad ametuhadithia: Abu Daawuud ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Zayd, ambaye amesema:
“Tulikuwa tukipita kwenye vikao tukiwa na Ayyuub ambapo tukawatolea salamu basi walikuwa wakijibu kwa sauti ya juu. Basi kana kwamba hilo lilikuwa ni adhabu.”
Abu Daawuud amesema:
“Kwa sababu ya kuchukia umaarufu.”
59 – Kwa njia hiyohiyo ametuhadithia Shujaa´: an-Nadhwr bin Shumayl ametuhadithia, kutoka kwa bwana mmoja ambaye amemtaja kwa jina, ambaye amesema:
”Ayuub alitoka safarini ambapo watu wengi wakamfuata. Akasema: “Lau si kuwa ninajua kwamba Allaah (´Azza wa Jall) anajua kutoka katika moyo wangu kwamba nachukia jambo hili, basi ningeliogopa ghadhabu ya Allaah (´Azza wa Jall).”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 78-84
- Imechapishwa: 22/01/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 78-84
Imechapishwa: 22/01/2026
https://firqatunnajia.com/08-lau-mgeyajua-tunayoyafanya-pale-tunapojifungia-milango/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket