08 – Kuomba msamah. Amesema (Ta´ala):
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ
“Basi elewa kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako.”[1]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Yule mwenye kulazimiana na kuomba msamaha basi Allaah atamfanyia njia ya kutokea katika kila dhiki, faraja juu ya kila simanzi na atamruzuku kwa njia asiyoitarajia.”[2]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika yale aliyopokea kutoka kwa Mola wake:
Ee mwanaadamu! Lau madhambi yako yangelifika kwenye mawingu ya mbingu kisha ukaniomba msamaha basi Ningelikusamehe.”[3]
Haya, ee dada wa Kiislamu, ndio bora ambayo unaweza kutumia muda wako. Hivyo basi, fanya hivo kwa wingi ili moyo wako uweze kupata utulivu. Amesema (Ta´ala):
أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ
“Zindukeni! Kwa kumtaja Allaah nyoyo hutulia!”[4]
[1] 47:19
[2] Abu Daawuud na Ibn Maajah. Ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´”, uk. 841 nr. 5829.
[3] at-Tirmidhiy (05/548) nr. 3540 ambaye amesema:
”Hadiyth hii ni ngeni. Hatuitambui isipokuwa kwa njia hii.”
[4] 13:28
- Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 17
- Imechapishwa: 09/02/2026
08 – Kuomba msamah. Amesema (Ta´ala):
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ
“Basi elewa kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako.”[1]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Yule mwenye kulazimiana na kuomba msamaha basi Allaah atamfanyia njia ya kutokea katika kila dhiki, faraja juu ya kila simanzi na atamruzuku kwa njia asiyoitarajia.”[2]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika yale aliyopokea kutoka kwa Mola wake:
Ee mwanaadamu! Lau madhambi yako yangelifika kwenye mawingu ya mbingu kisha ukaniomba msamaha basi Ningelikusamehe.”[3]
Haya, ee dada wa Kiislamu, ndio bora ambayo unaweza kutumia muda wako. Hivyo basi, fanya hivo kwa wingi ili moyo wako uweze kupata utulivu. Amesema (Ta´ala):
أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ
“Zindukeni! Kwa kumtaja Allaah nyoyo hutulia!”[4]
[1] 47:19
[2] Abu Daawuud na Ibn Maajah. Ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´”, uk. 841 nr. 5829.
[3] at-Tirmidhiy (05/548) nr. 3540 ambaye amesema:
”Hadiyth hii ni ngeni. Hatuitambui isipokuwa kwa njia hii.”
[4] 13:28
Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 17
Imechapishwa: 09/02/2026
https://firqatunnajia.com/08-kumuomba-allaah-msamaha/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket