08. Kujitenga mbali na kurushiana maneno, mijadala ya mizozo ya kidini

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tunaonelea kuwa Sunnah imejengwa juu ya kushikamana na yale waliyokuwemo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaiga, kujiepusha na Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu, kujiepusha na mizozo, kukaa na Ahl-ul-Ahwaa´ na kujiepusha na kurushiana maneno, mijadala na ugomvi katika dini.”

MAELEZO

Dalili ya hilo ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

“Wala msiwe miongoni mwa washirikina; miongoni mwa wale walioifarikisha dini yao wakawa makundi makundi. Kila kundi wanafurahia yale waliyomo.”[1]

مَا يُجَادِلُ فِي آيَاتِ اللَّـهِ إِلَّا الَّذِينَ كَفَرُوا

”Habishani katika Aayah za Allaah isipokuwa wale waliokufuru.”[2]

مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ

”Hawakukupigia mfano huo isipokuwa tu kutaka kubisha. Bali wao ni watu makhasimu.”[3]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna watu waliopotea baada ya uongofu waliokuwemo isipokuwa baada ya kuanza mijadala.”[4][5]

“Watu wanaochukiwa na Allaah zaidi ni wale wapotevu mabingwa wa kujadili.”[6]

´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) amesema:

“Atakayeifanya dini yake ni sehemu ya mabishano atabadilika sana.”[7]

al-Hasan alimwambia mtu ambaye alikuwa anataka kujadiliana naye:

“Kuhusu mimi naielewa dini yangu. Ikiwa wewe umeipoteza dini yako nenda ukaitafute.”

[1] 30:31-32

[2] 40:04

[3] 43:58

[4] at-Tirmidhiy (3253) na Ibn Maajah (48). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (14).

[5] al-Bukhaariy (2457) na Muslim (2668).

[6] ad-Daarimiy (312) na Ibn Battwah katika ”al-Ibaanah al-Kubraa” (565).

[7] Ibn Battwah katika ”al-Ibaanah al-Kubraa” (586).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 81-82
  • Imechapishwa: 11/02/2017