Kwa mujibu wa Hadiyth hii kufunga Ramadhaan kunathibiti kwa njia mbili:

1 – Kuonekana kwa mwezi mwandamo wakati wa magharibi katika usiku wa kwanza wa Ramadhaan.

2 – Kumaliza mwezi wa Sha’baan kuwa siku thelathini ikiwa mwezi mwandamo haukuonekana.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mkiuona fungeni na mkiuona fungueni.”

Hii ni kanuni kubwa kwamba mwanzo wa mwezi hujulikana kwa ishara ya wazi, ambayo ni kuonekana kwa mwezi mwandamo. Kufunga kumefungamanishwa na kuonekana mwezi mwandamo na kufungua pia kumefungamanishwa na kuonekana mwezi mwandamo.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/436-437)
  • Imechapishwa: 16/02/2025